MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupita chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amesema kuwa mkakati wake ni kuwainua kiuchumi wanawake wa UWT mkoa wa Iringa kwa kuwawezesha kiuchumi ili waendelee kufanya shughuli za kuzalisha bidhaa mbalimbali za kukuza uchumi.
Akizungumza kwenye baraza kuu la UWT mkoa wa Iringa,mbunge Rose Tweve alisema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa wakijitumia katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikichangia kukuza uchumi wa familia na kukuza maendeleo ya nchi.
Alisema kuwa kwa miaka mitano ya ubunge wake atajikita kuhakikisha anawaezesha wanawake wa UWT kiuchumi ili kuhakikisha anakuza uchumi wako kwa kuwatumikia vema katika eneo hilo ambalo yeye anaona ndio suruhu ya kuwa komboa wanawake kiuchumi.
“Ukienda saizi sokoni,shambani,madukani,kwenye miradi midogo,vikundi vingi vya kimaendeleo ni wanawake hata vijiweni utawakuta wanawake hivyo mimi nitajikita kuhakikisha nawawezesha wanawake kiuchumi” alisema Rose Tweve
Alisema kuwa ataendelea kuhakikisha vikundi vya wanawake vinapata mikopo ambayo inatolewa na Halmashauri kwa kuwa ni wajibu wake katika shughuli za kibunge kwa kuwa alichaguliwa na wanawake wa mkoa wa Iringa.
Rose alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitano kwa ushirikiano mbunge mwezake Nancy Nyalusi watatoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila kikundi cha UWT mkoa wa Iringa kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawakomboa kiuchumi wanawake wa mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (NEC) kupitia mkoa wa Iringa Salim Abri Asas alisema kuwa ataendelea kuwaunga mkono UWT kupitia vikundi vilivyoanzishwa na mbunge Rose Tweve toka alivyochaguliwa kwa mara ya kwanza hadi sasa vimeonyesha uhai katika kukuza uchumi.
Alisema wanawake wa umoja huo wanatakiwa kuwa na uchumi mzuri ili waweze kufanya vizuri shughuli za kisiasa ambapo wamekuwa msaada mkubwa kwenye chama cha mapinduzi katika nyakati zote ziwe za kichaguzi au kukuza chama wamekuwa mstari wa mbele.
Asas alisema kuwa haiwezekani kila wakati wanawake wa UWT wanakuwa tegemezi hivyo amewataka kuandaa miradi ya kimkoa na kila wilaya iwe na mradi mkubwa ambao utawakomboa kiuchumi kwa kuwa jumuiya hiyo bado haijajikwamua kiuchumi.
Asas aliwataka UWT mkoa wa Iringa kuhakikisha inawashirikisha wachumi katika kubuni miradi ambayo itakuwa na manufaa kwenye umoja huo kwa miaka mingi ijayo.
Post a Comment