Featured

    Featured Posts

MURUSURI AWAPIGA MSASA WANAFUNZI UDSM AFRIKA KUACHA UTEGEMEZI IIMARISHE 'RESOURCE MOBILIZATION'

 TANZANIA na Afrika itaweza kuondoa kabisa utegemezi kwa mataifa makubwa kiuchumi duniani iwapo uwezo wa "resource Mobilization,' utaimarika nchini na katika mataifa haya.


" resource mobilization ni muhimu sana kwa maendeleo ya mataifa yetu kwani hata raslimali tunazosaidiwa na mataifa makubwa kiuchumi duniani, yaani wafadhili, zinatokana na maarifa haya," alisema Bw. Derek Murusuri kutoka CTG Resources Limited, alipokuwa akiwasilisha mada kama "Guest Speaker" kwa wanafunzi wa uzamili, wanaochukua kozi ya usimamizi wa miradi (Project Management) katika Idara ya Jiografia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo (23 Julai, 2021).

Murusuri aliyepata kuwa Meneja wa Biashara na Mapato wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), aliwaambia washiriki hao kuwa resource mobilization ni mhimili wa taifa lolote duniani linalotaka kufikia maendeleo makubwa. "Tunahitaji wataalamu wengi kwenye maarifa haya ili kuleta mabadiliko makubwa kiuchumi na kijamii," alisema.

Naye Mratibu wa kozi hiyo yenye utaalamu adhimu unaokita mizizi katika bara la Afrika hivi sasa, Dkt. Zablon Kengera, amesema kozi hiyo ambayo ilianzishwa takriban miaka nane iliyopita, imewavutia wanafunzi wengi wanaosoma jioni baada ya majukumu yao ya kikazi.

Wengine waliowasilisha mada katika Warsha hiyo iliyokuwa ikiwaandaa wanafunzi hao kwenda katika mafunzo ya vitendo ni Erick Chrispin wa True Maisha, Vivian Kazi wa ESRF, Clement Kisinga wa NIMR, Barnabas Lupande na mwakilishi wa Mkurugenzi wa ILO nchini.

Akifunga mafunzo hayo, aliyepata kuwa Mkuu wa Idara hiyo, Dr. Cosmas Sokoni, amewataka washiriki wa Warsha hiyo kuzingatia maarifa waliyopewa kutoka kwenye "industry" baada ya kufundishwa nadharia.

Kozi hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya bara la Afrika ambalo limekuwa na changamoto ya usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Bw. Derek Murusuri, aliyepata kuwa resource mobilization manager wa iliyokuwa Tanzania Media Fund (TMF), sasa Tanzania Media Foundation, akiwasilisha mada inayohusu umuhimu wa resource mobilization kwa maendeleo kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili ya project management, siku ya ijumaa 23 Julai, 2021 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana