Mwekezaji katika Kiwanda Cha kutengeneza nguzo za umeme Cha Lesheye Investment Company Ltd, Dkt. Emil Woiso akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mwekezaji katika sekta viwanda vya kutengeneza nguzo za umeme amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ruhusu Hassan kuwasidia ili waweze kuendelea kuzalisha nguzo za umeme katika mazingira rafiki kwa ajili ya kukuza uchumi wa viwanda kwa Maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwekezaji katika Kiwanda Cha kutengeneza nguzo za umeme Cha Lesheye Investment Company Ltd, Dkt. Emil Woiso, amesema kuwa wadau wa viwanda vya kutengeneza nguzo za umeme kwa sasa wapo katika wakati mgumu kwani wamekuwa wakipewa maagizo Mamlaka husika ambayo yanakwenda kukwamisha uzalishaji wa viwanda.
Dkt. Woiso amesema kuwa wameambiwa kwa sasa wanunue mitambo wa kukausha nguzo za umeme jambo ambalo linaonekana ni changamoto kwao kutokana mitambo hiyo inauzwa fedha nyingi.
“Gharama za kununua mitambo ya kukausha nguzo ni mamilioni ya fedha, hivyo tutashindwa kununua, na hii inaonekana kuna watu wanataka kutufanyia hujuma kutoka wakati tunaaza kazi hawajatupa masharti kama hayo” amesema Dkt. Woiso.
Dkt. Woiso ambaye ni mtumishi wa Mungu amefafanua kuwa kabla ya kufanya uwekezaji waliambiwa na Hayati Dkt. Magufuli kuwa nguzo za umeme Serikali haitaagiza kutoka nje ya nchi badala yake wawekezaji wa ndani watapewa nafsi ya kuzalisha kupitia viwanda vyao.
“Baada ya Hayati kuondoka kuna nguvu kubwa ambayo inataka kuagiza nguzo za umeme kutoka nje ya nchi kwa mafunaa yao binafsi kutokana wameaza kutuwekea vikwazo ambayo vinapelekea kwenda kuzalisha nguzo ambazo zitaonekana hazina ubora” amesema Dkt. Woiso.
Ameeleza kuwa ni busara Mawaziri wenye dhamana waitishe kikao wadau wote wanaotengeze nguzo za umeme ili wajadili kwa pamoja na namna ya kusonga mbele kuliko kurudi nyuma kwenda kununua nguzo za umeme nje ya nchi.
Dkt. Woiso amebainisha kuwa kuna mashamba makubwa ya miti ambayo wadau wamelima kwa ajili ya nguzo za umeme kwa ajili ya kukuza uchumi wa viwanda hapa nchini.
Katika hatua nyengine Mwekezaji huyo amebainisha baadhi ya watendaji wa serikali wamechukua majengo yake kinyume na taratibu yaliyopo Mwenge Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa amekuwa akiishi katika majengo hayo tangu mwaka 1979 na kufanikiwa kujenga jengo kubwa kwa mkopo wa shillingi bilioni mbili kwa ajili ya wawekezaji kutoka nchi ya nchi.
“Nimesikitishwa sana kwa sababu wanataka kunipokonya hati miliki na majengo yangu yote kitu ambacho sio utaratibu, tunajua Rais wetu ni msikivu sana na tunauwakika atatusikia na kutusaidia” amesema Dkt. Woiso.
Post a Comment