Akizungunza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru wailayani Bahi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kuwa ukiwa mkoani Dodoma utaweka mawe ya msingi, kuzindua, kutembelea na kukabidhi miradi mbalimbalimbali yenye thamani ya zaidi ya sh. bil. 41.
Baada ya kukimbizwa katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma ambazo ni; Bahi, Chemba, Kondoa, Chamwino, Kongwa, Dodoma Mjini na Mpwapwa utakabidhiwa Mkoa wa Morogoro.
Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa Mwenge utaweka mawe ya msingi, kudinduliwa, kutembelewa miradi yenye tahamni ya sh. blioni 1.9. Baada ya hapo utakabidhiwa utakabidhiwa katika Wilaya ya Chemba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akikabidhi taarifa ya mkoa wakati wa kukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dodoma. |
Baadhi ya wakuu wa Wilaya na viongozi wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Seleman Mwenda. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga akiiupokea Mwenge wa Uhuru. |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mtaka akisoma taarifa ya mkoa huo.
Mwenge wa Uhuru ukipokelewa na wakuu wa vyombo vya Dola.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment