Na Richard Mwaikenda, Dodoma
TAASISI ya Pass Trust inayojihusisha na Uendelezaji wa Kilimo, imekubali ombi la kufungua ofisi Makao Maku ya nchi Dodoma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Maonesho ya Pass Trust, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Dkt. Taus Kida,alisema licha kuwa na ofisi ya uatamizi wilayani Kongwa, wana mpango wa kufungua ofisi ya kisasa jijini Dodoma.
Dkt. Tausi amekubali ombi hilo lililotolewa na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma walioishauri taasisi hiyo kuwa kuna umuhimu wa taasisi hiyo muhimu kwa wakulima kufungua ofisi makao makuu Dodoma kwa lengo la kuboresha kilimo na hasa zao la mkakati la zabibu.
"Pass njooni Dodoma tuna vikundi vingi na vyama vya ushirika vipo ili muviunganishe na vyombo vya fedha, lakini pia naomba muwe karibu na ofisi ya mkoa mratibu jinsi ya kufanya mikutano na wawakilishi wa wananchi madiwani katika Kata 41 za jiji la Dodoma, " amesema Pinda maarufu kama Mtoto wa mkulima.
Amesema ujio wa Pass mkoani humo utawafanya wakulima kupata mitaji kwa kuwaunganisha na taasisi za fedha, lakini pia kulima kisayansi na maarifa hivy kupata mafanikio mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kuwa ujio wa Pass Trust utaamsha kilimo biashara Dodoma na Kanda ya Kati, lakini pia kuwa wadau wakubwa wa zao la kimkakati la zabibu.
Post a Comment