Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika tume hiyo, Richard Cheyo ametoa takwimu hizo leo Ijumaa (Julai 2, 2021) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Cheyo alisema tume hiyo ilijadilia na kutoa uamuzi wa rufaa hizo 107 ambapo kati ya hizo, 76 zilikataliwa huku 12 zilikubaliwa kwa masharti kuwa mashauri hayo yaanzishwe upya kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
“Rufaa 10 zilikatwa nje ya muda, hivyo zilitupiliwa mbali na tume. Pia tume ilipokea na kutolea uamuzi malalamiko nane kati ya hayo malalamiko matatu yalikataliwa. Malalamiko matano yalikubaliwa bila masharti,” alisema.
Alitaja baadhi ya mambo ambayo yaliwaingiza watumishi hao katika mashauri hayo ni pamoja na utoro kazini kwa zaidi ya siku tano bila ruhusa ya mwajiri, watumishi kwenda masomoni bila ruhusa ya mwajiri na kutoa taarifa za uongo kwa mwajiri.
Mengine, mwa mujibu wa Cheyo, ni kuajiriwa katika utumishi wa umma bila kuwa na sifa na kughushi cheti cha uhitimu wa elimu ya kidato cha nne na kushindwa kuwasilisha cheti cha kidato cha nne.
Alibainisha kuwa kukosa uaminifu, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha ya umma pamoja na uzembe uliokithiri na kushindwa kutekeleza majukumu ni makosa mengine yaliyowaingiza watumishi hao matatani.
Cheyo alisema katika kipindi cha miaka miwili 2019/2020 na 2020/2021, Tume imeshughulikia na kutoa rufaa 626 kati ya hizo, 219 zilikubaliwa, 227 zilikataliwa na 180 zilikatwa nje ya muda.
Post a Comment