Featured

    Featured Posts

WASIOVAA BARAKOA MARUFUKU KWENDA KUWAONA WAGONJWA HOSPITALI ZOTE ZA DODOMA:RC MTAKA

Mganga Mfawidhi wa Hospitari ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest, akielezea kuhusu uwezo wa mitambo ya kutengeneza hewa ya Oksijeni  kwa ajili ya tiba ya wagonjwa wa  Corona na magonjwa mengineyo iliyopo hospitalini hapo.

Dkt. Ernest amaeishukuru serikali kununua matambo huo wenye thamani ya sh. bil. 1.2 amabo umesaidia sana kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya upumuaji corona na wagonjwa wengine.

Hivi sasa hospitali hiyo ina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa wenye matitizo hayo 200 kwa pamoja lakini hadi sasa wanahudumia wagonjwa 29 kutokana na kwamba  hivi sasa hakuna msongamano.

Dkt.  Ernest amesema hivi sasa kupitia matambo huo wana mpango wa kuweka kila wodi nakila kitanda kuweka  Flow meter ya hewa ya oksijeni.
Baadhi ya mitambo ya kufua hewa ya oksijeni yenye thamani ya sh. bilioni 1.2  iliyopo hosptalini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka 

 

Baadhi ya waandishi wa habari (waliosimama)
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest akiwaonesha waandishi wa habari kifaa kinachopima wingi wa hewa ya oksijeni katika mwili wa binadamu katika kitengo cha dharula.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Best Magoma akielezea mpango wa kusambaza huduma ya hewa ya oksijeni katika hospitali mbalimbali za mkoa huo.

Dkt Ernest akionesha sehemu yenye 'Flowmeter' ya hewa ya oksijeni ikiwa ni moja kati ya zilizowekwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.

Dkt Ernest akionesha Flowmeter  zilizowekwa kwenye vitanda vya wagonjwa katika wodi  namba 13 na 14 hospitalini hapo.



Sehemu ya mapokezi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.




Na Richard Mwaikenda, Ccm Blog, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amewataka wananchi wanaokwenda kuwaona wagonjwa katika hospitali hizo kuhakikisha wanavaa barakoa kwa lengo la kujikinga wao na wagonjwa dhidi ya ugonjwa wa Corona ama sivyo wasiruhusiwe.

Ametoa tahadhari hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliojionea mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni  inayosambazwa katika wodi mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

RC Mtaka ametoa amri ya kutowaruhusu watu wote wanaokwenda kuwafariji wagonjwa ama kuwapelekea chakula wasiovaa barakoa katika hospitali za binafsi na za serikali mkoani humo.


"Mganga Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wanaokwenda kumuona mgonjwa wasizidi watu watatu, sisi wa mkoa tumeyapokea lakini nyongeza yake ni ukitaka kwenda kumuona mgonjwa, kumpelekea chakula bila kuvaa barakoa hatutakuruhusu, ili uruhusiwe kumuona kwenye zahanati, kituo cha afya, hospitali ya serikali au ya binafsi tunawaomba mvae barakoa kwa faida yako na mgonjwa pia," amesisitiza RC Mtaka.

Pia ameweka msisitizo kwa maeneo yote ya biashara na yenye mikusanyiko mikubwa, sokoni, minada na stendi kila mmoja achukue tahadhari kwa kuvaa  barakoa na kunawa maji tiririka ama kujipaka sanitaiza.

Amewashauri watu wote wanaojihisi kuwa na dalili za ugonjwa wa corona wasibahatishe kuhusu tiba bali waende kwenye zahanati, vituo vya afya  na hospitali kupimwa  ili kuwa na uhakika.

Vilevile amezitaka daladala kupakia 'level seat' na bodaboda kuzingatia sheria ya kupakia abiria mmoja ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo.

RC Mtaka, amekiri uwepo wa wagonjwa wa corona mkoani humo na kwamba  wanajitosheleza kuwahudumia kwa vile hakuna msongamano.







author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana