Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda (kulia), akimkabidhi ufunguo Anthony Maganga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 ikiwa ni mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia), akimkabidhi namba yAnthony Maganga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda, akimkabidhi ufunguo Lillian Maricky wa Kampuni ya Magic LN Suppliers ya Chalinze, mkoani Pwani ikiwa ni ishara ya kumkabidhi mitambo ya kuvuna mpunga yenye thamani ya sh. mil.79 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda (kulia), akimkabidhi ufunguo Gebe Millinga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya John Deere pamoja na majembe yake lenye thamani ya sh. mil. 71.4 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida. Gebe amepokea trewkta hilo kwa niaba ya kaka yake Mwanzo Millinga anayefanya kazi ya kilimo mkoani Ruvuma.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda akimkabidhi ufunguo Dickson Tesha ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland lenye thamani ya sh. mil. 46 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Tesha amepokea trekta hilo kwa niaba ya Japhet Ndebesi wa Chamwino, mkoani Dodoma.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolph Mkenda amezindua Kampuni ya Pass Leasing ya kukopesha wakulima zana za Kilimo bila dhamana na kwa riba nafuu.
Baada ya kuzindua amekabidhi zana za kilimo za kisisa kwa wateja wanne wa kwanza ambazo ni matrekta matatu na mtambo wa kuvunia mpunga.
Waliokabidhiwa ni; Kampuni ya Magic LN Suppliers ya Chalinze mkoani Pwani ambayo imekopeshwa mtambo wa kuvunia mpunga wenye thamani ya sh. Mil. 79, Anthony Maganga wa Igunga Tabora aliyepata Trekta aina ya New Holland lenye thamani ya sh. Mil. 54.
Wengine ni Japhet Ndebezi wa Chamwino mkoani Dodoma aliyekopeshwa Trekta lenye thamani ya sh. Mil. 46 na Mwandishi wa Habari Mwanzo Millinga wa Ruvuma ambaye amepata Trekta aina ya John Deere pamoja na majembe yake lenye thamani ya sh. Mil. 71.4.
Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na viongozi wa Taasisi Pass Trust pamoja na wananchi waliohudhuria Wiki ya Pass Trust kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mikopo inayotolewa na Kampuni ya Pass Leasing kwa upande wa kilimo ni; zana za kuwezesha uzalishaji wa kilimo cha mazao, usindikaji, uhifadhi wa mazao na usafirishaji.
Kwa upande wa uvuvi ni; vifaa uvuvi na mashine zote zitumikazo kuongeza tija katika sekta ya uvuvi. Ufugaji nyuki ni; Vifaa mbalimbali vya kuongeza tija na thamani katika sekta ya nyuki na mazao yatokayo na na nyuki.
Ufugaji ni; Vifaa na mashine za kuongeza tija katika sekta ya ufugaji na kwa upande wa misitu ni vifaa na mashine zitumikazo kwenye misitu na viwanda vya mbao.
Post a Comment