Featured

    Featured Posts

ZIARA YA MWENYEKITI WA UWT DAR YAZIDI KUZAA MATUNDA, WILANI ILALA YAINGIZA MICHANGO YA SH. MILIONI 6.2 ZA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akizungumza na Viongizi wa UWT na CCM katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM, Wilaya ya Ilala, jana ikiwa ni mwendekezo wa ziara alizozianza hivi karibuni kutembelea wilaya zote za mkoa huo. (Picha na Bashir Nkoromo).


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Ziara za Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga katika wilaya za mkoa huo, imeendelea kuzaa matunda baada jana kuingiza jumla ya Sh. Milioni 6,200,000 zilizochangwa katika mkutano wake Wilayani Ilala, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT katika mkoa huo.


Katika ziara hizo ambazo Mwenyekiti huyo anaambana na Kamati ya Utekekezaji ya UWT mkoa, zinalenga kuwashukuru Wanachama wa UWT kwa kumchagua, kuimarisha Uhai wa Jumuiya na Chama na kufanya harambee katika mikutano wakati wa ziara hizo kwa ajili ya kupata fedha na vifaa kwa ajili ya kutimiza azma ya kujenga nyumba 5 katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam na moja ngazi ya mkoa za Watumishi wa UWT.


Akiyangaza kilichopatikana baada ya harambee, katika mkutano wa ziara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala na kuhudhuriwa na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa UWT na wa CCM), Katibu wa UWT mkoa Grace Haule alisema kiasi hicho kilichopatikana cha Sh. Milioni 6.6,  sh. 600,000 ni fedha taslimu na ahadi sh. milioni 5.6.


Grace alisema mbali na michango ya fedha pia katika harambee hiyo zilipatikana ahadi za michango ya matofali 2,900 na nondo tani moja.


Baada ya kutangaza kilichopo Grace alifafanua namna ya viongozi kuhifadhi fedha za Jumuiya hiyo ili ziweze kuwa salama na kutumika vema kulingana na malengo yaliyokusudiwa.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa UWT mkoa Florence Masunga Jumuita hiyo mkoa wa Dar es Salaam, imepanga kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa ajili ya Watumishi wake Novemba mwaka huu kwa gharama ya Sh. Bilioni 1.3, kwa nyumba zote.


"Tumeamua tuanze kuchangishana wenyewe kwenye mikutano ya ziara zetu, baadaye ndiyo tutashirikisha wadau wengine kutuchangia pale tutakapokuwa tumeoelewa", amesema Florence Haule


Akizungumza na Wanachama, Watendaji na Viongozi wa UWT na CCM kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, aliuelezea kwa kina mpango wa ujenzi wa nyumba hizo, akisema zitakuwa zenye hadhi ya kisasa na stahili bora kwa kuishi mtumishi wa Jumuiya hiyo.


Florence aliwataka Wanachama wa Jumuiya hiyo, kupambana katika uchangiaji fedha za ujenzi wa nyumba hizo ili kuudhihirishia umma kwamba Wanawake wanaweza na wakiwa na jambo lao haikwami.


Alisema, pamoja na lengo kuu la ziara zake katika wilaya zote kuwa ni kuhamasisha uchagiaji wa ujenzi wa nyumba hizo, lakini pia ni kuwahamasisha Wanawake kuzitumia fursa za mikopo zilizopo ili kuinua vipato vyao, familia zao na taifa kwa jumla.






N



N
N



N
N
N
N
N
N

N
N
N

N
N
N
N

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana