Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Dk. Phillis Nyimbi ametoa mwito kwa Wanawake kuchangamkia fursa nzuri zilizowekwa na Serikali za Chama Cha Mapinduzi CCM) kwa ajili ya kuwainua kiuchumi, ikiwemo mikopo isiyo na riba kupitia Halmashauri mbalimbali zilizopo hapa nchini.
Pia amewa amewataka Wanawake wote nchini hususan wa Jumuiya hiyo kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuchapa kazi kwa bidii na iliyotukuka ili aweze kufanikisha malengo na maono makubwa aliyonayo katika kulivusha taifa la Tanzania kwenda mbele zaidi.
Dk. Nyimbi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasmi ofisi na Katbu Mkuu wa awali wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, jana.
"Wanawake hatuna haja ya kuhangaika kuitafuta shilingi ilipo, Serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan imeweka fursa nyingi kwa ajili ya kumuinua mwanamke kiuchmi, ikiwemo mikopo isiyo na riba kupitia Halmashauri mbalimbali, kwa hiyo jambo la msingi hapa ni sisi wanawake kuhamasishana ili kuzichangamkia fursa hizo, na ninaamini tukizitumia fursa hizi vizuri tutainuka kiuchumi kwa manufaa yetu na taifa letu kwa jumla", Alisema Dk. Dk. Phillis Nyimbi
"Namshukuru kwa dhati Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naishukuru Kamati Kuu ya CCM na pia naishukuru Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo kwa kuonyesha imani kwangu na kuniteua kushika nafasi hii, naahidi nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kuitendea haki imani hii niliyopewa.
Nitashirikiana na wenzangu kuhakikisha kwamba tunaendelea kuimarisha Jumuiya yetu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunaendelea kusimamia ipasavyo utekelezaji wa Ilani ya CCM, nina imani kwa kufanya hayo tutakuwa tumerahisisha majukumu mbalimbali ambayo Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu Samia Suluhu Hassan anayafanya", Alisema Dk. Phillis Nyimbi
Aliwataka wanawake wa UWT na wengine wote kwa jumla hapa nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili mipango na maono makubwa aliyonayo kwa Taifa la Tanzania yaweze kukamilika vilivyo kwa ajili ya manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadaye.
"Mwenyekiti wetu wa CCM ambaye pia ni Rais wetu ana mipango na maono makubwa katika nchi yetu na mengi tunayashuhudia, ikiwemo hili la kutotubagua sisi wanawake katika nafasi za uongozi na mambo mengi yahusuyo mustaakabali wa nchi, kisiasa, kiuchumi na kijamii."
Sasa kwa mfano katika hili la kutupa imani kwa kutotuacha wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi, lazima mjue kuwa anatupa nafasi hizi siyo kwa sababu tu sisi ni wanawake wenzake hapana, anatupa nafasi hizi ili tuendelee kumsaidia ili hatimaye kwa pamoja tulete tija katika maeneo hayo anayotuweka kwa maslahi ya taifa letu, na kwa kufanya hivyo ndiyo wanawake tutakuwa tumetoa mchango wetu katika kumuunga mkono rais katika kutekeleza maono na mipango yake mikubwa kwa taifa hili", Alisema Dk. Phillis Nyimbi
Kuhusu changamoto ndani ya UWT, Dk. Philipe alisema, anatambua zipo kwa kuwa siyo rahisi taasisi kubwa kama UWT kawa haina changamoto ndani ya mafanikio iliyonayo, lakini akasema atashirikiana na wenzake kuleta achachu ya kuendelea kuijenga na kuiimarisha Jumuiya hiyo katika njyanja mbali mbali hasa kiuchumi, kisiasa.
Dk. Philipe alimshukuru mtangulizi wake Queen Mlozi akimwelezea kuwa ni mwanamke jasiri na mchapakazi, na kumshukuru kwa kumkabidhi ofisi katika mazingira ya furaha na upendo.
Mapema Katibu Mkuu mstaafu wa UWT alimpongeza Dk. Phillis Nyimbi kwa kuaminiwa na Chama na kuteuliwa kuwa Katbu Mkuu mpya wa UWT na kuwaomba watumishi wa Jumuiya hyo katika ngazi zote kumpa ushirkiano wa dhati katika majukumu yake kama walivyokuwa wakimpatia yeye ushrikiano wakati wa uongozi wake.
Makabidhiano
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dk. Phillis Nyimbi (Kushoto) akikabidhiwa vitendea kazi na aliyekuwa Katibu Mku wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, wakati wa makabidhiano rasmi ya ofisi yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.Aliyekuwa Katibu Mku wa UWT Queen Mlozi, akisainia nyaraka mbalimbali za makabidhiano, wakati wa makabidhiano hayo rasmi ya ofisi na Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo Phillis Nyambi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Katibu Mkuu mpya wa UWT Dk. Phillis Nyambi, akisainia nyaraka mbalimbali za makabidhiano, wakati wa makabidhiano hayo rasmi ya ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Mwanasheria wa UWT Mariam Msangi akisaini kuwa shahidi, nyaraka mbalimbali za makabidhiano, wakati wa makabidhiano hayo rasmi ya ofisi na kati ya Katibu Mkuu mpya wa UWT Dk. Phillis Nyambi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Maudline Castiko, akisaini kuwa shahidi, nyaraka mbalimbali za makabidhiano, wakati wa makabidhiano hayo rasmi ya ofisi na kati ya Katibu Mkuu mpya wa UWT Dk. Phillis Nyambi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mku wa UWT Queen Mlozi, akizungumza wakati wa hafla ya rasmi ya ofisi na Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo Phillis Nyambi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Katibu Mkuu mpya wa UWT Dk. Phillis Nyambi, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo rasmi ya ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo Queen Mlozi, yaliyofanyika jana, Makao Makuu ya UWT, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma. (Picha zote kwa hisani ya UWT mkoa wa Dar es Salaam).
Post a Comment