CCM Blog, Dar es salaam
Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) kilichopo katika Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Nganga Nkonya amenusurika kufukuzwa kazi na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda kutokana kubainika kuwa kulikuwa na hujuma za kiutendaji katika mfumo BPS na hivyo kusababisha kuchelewa kwa upatikanaji wa mbolea kwa wingi na kwa wakati.
Badala ya kufukuwa kazi Waziri Mkenda ameagiza Kaimu Meneja huyo kuondolewa BPS na kuhamishiwa Wizarani kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine huku akifafanua kuwa miongoni mwa hujuma zilizobainika ni kuwa kulikuwa na mtu anajaribu kucheza na mfumo huku msimamizi huyo akishindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa matakwa ya serikali ya kuhakikisha wakulima wanapata mbolea ya kutosha na kwa wakati.
Hayo yamejiri leo wakati Waziri Mkenda alipokuwa akizungumzai na wafanyabiashara ya mbolea katika Mkutano wake na wafanyabiashara hayo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, ambao ulitumika kujadili masuala mbalimbali kuhsu biashaya hiyo ikiwemo kutafuta namna itakayosaidia kushusha bei ya bidhaa hiyo.
" Huyu kwa kweli nilikuwa nimfukuze kazi, lakini nimeamua animeagiza aondolewe pale BPS aje Wizarani apangowe kazi nyingine, maana sisi suala la mbolea ni la kufa na kupona sio suala la mzaha kama alivyokuwa anafanya huyu, maana hata namba ya mawasiliano ilikuwa imewekwa kwamba ndiyo itumike lakini umbe siyo ya ofisi. ni ya mtu binasi wa huko mikoani", alisema Waziri Mkenda
Alisema, katika kutafuta njia ya kupungua bei ya mbolea serikali imeondoa utaratibu wa zamani uliokuwa ukitumika ambao ulikuwa hauleti ushindani, na sasa serikali imeweka utaratibu mpya ambao utaleta ushindani kwa kuwa sasa mfanyabishara ataruhusiwa kununua kiasi chochote cha mbolea kutoka nje na pia ataruhusiwa kuuza kokote ikiwemo nje ikiwa atapenda kutofautiza na utaratibu wa awali ambapo wafanyabishara walikuwa hawaruhisiwi kuuza mbolea nje ya nchi
Waziri Mkenda alisema, iili kilimo kiendelee inahitajika tekolojia ya kisasa hasa katika suala la mbolea hivyi serikali itaendelea kufanya mapitio ya mfumo uliopo na kutafuta namna nzuri ya kumsaidia mkulima kwa ajili ya upatikanaji wa mbolea.
Kuhusu bei ya mbolea kupanda, Waziri Mkenda amesema kuwa hilo ni tatizo la Dunia nzima kwani katika soko la Dunia bei ya mbolea imepanda kwa kiasi kikubwa mbali nagharama za usafirishaji.
Ameeleza kuwa pia tayari Serikali imeielekeza Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) kuanza kutoa vibali vya kuuza mbolea ambayo imeshaingia nchini (Export Permit) badala ya vibali hivyo kutolewa ofisi ya Waziri wa Kilimo.
Ili kuongeza ufanisi zaidi wa utendaji Waziri Mkenda amesema kuwa vibali hivyo vitatolewa kwa njia ya mtandao (Online) badala yake Ofisi ya Waziri wa Kilimo itakuwa na jukumu la kupewa taarifa ya utekelezaji wa utoaji vibali uliofanywa na TFRA.
Aidha Waziri Mkenda amesema Serikali inafanya mpango kwa kulifufua Shirika la Mbolea (TFA) ili liweze kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uagizaji mbolea kutoka nje ya nchi na uuzaji ndani na nje ya nchi.
Post a Comment