Na Lydia Lugakila, Bukoba
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imeshika nafasi ya mwisho kwa ukusanyaji wa kodi Kati ya wilaya nane za mkoa huo.
Meya wa Manispaa hiyo Godson Gypson, amesema hayo katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata yake, kilichofanyika katika Uwanja wa Kaitaba, jana.
Akizungumzia hali hiyo ya ukusanyaji kodi amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa hiyo imekuwa ya mwisho katika kukusanya kodi katika wilaya hizo nane hali ambayo imesababisha kudhoofisha maendeleo.
"Sasa tuache siasa tukusanye kodi, Mkurugenzi nahitaji mapato sihitaji maneno, tukusanye kodi kwa mujibu wa sheria" alisema Mstahiki Meya Godson huku akiwaomba madiwani kusimamia kuzungumzia suala la ukusanyaji mapato Katika kata zote 14.
Amesema ulipaji kodi sio wa kubembeleza hivyo kwa mujibu wa sheria lazima kodi ilipwe ili kupata maendeleo Katika manispaa hiyo na kuwaomba wananchi pamoja na mdiwani kuwa tayari kushiriki kuchangia miradi ya maendeleo na kuwa hawawezi fanya maendeleo bila kukusanya kodi huku akiahidi halmashauri hiyo kufanya vizuri katika ukusanyaji kodi kwa awamu ijayo kwani tayari wamejipanga ipasavyo.
Meya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Godson Rwegasira Gypson akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani
Post a Comment