Mziwanda Chimwege
Mgombea nafasi ya Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Mziwanda Chimwege naomba Kura zenu za Ndiyo ili nikasimamie na Kutekeleza Misingi ya Haki kati ya Watumishi na Waajiri.Chimwege; ameyasema hayo mapema kabla ya kuingia ukumbini huku akitetea kiti chake leo Agosti 27, 2021 ambapo uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Posta Jijini Dar es Salaa Saa 3 Asubuhi ya leo akichuana na Brendan Maro na Jemse Albart na kuomba ridhaa yakumalizia viporo ambavyo angependa avimalizie na kuomba kwa mara nyingine na akitaja aliyoyafanikisha katika Uongozi wake ni.
(1).
Kujenga mahusiano sehem za kazi kati ya matawi na Waajiri.
(2).
Kuanzisha semina za viongozi wa matawi na Waajiri 2018 Mtwara.
(3).
Kuendesha Semina Jijiji Mwanza 2021.
(4).
Kusikiliza na kutatua migogoro ya wanachama na Viongozi wa Tawi la Mahakama Kuu.
(5).
Kusikiliza na kutatua mgogoro kati ya viongozi wa Chama cha TUGHE wa Uwanja wa Ndege Mwalimu Nyerere na Mamlaka ya Hali ya Hewa viwanja vya Ndege (TCAA)
(6).
Kuandaa Semina ya Viongozi na Waajiri Jijini Mbeya 2021.
Mwisho napenda kuomba kura zote kwangu. Asanteni
Post a Comment