Featured

    Featured Posts

PROF. MKENDA AIPONGEZA UVCCM ROMBO KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WAKATI WA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA

Mbunge wa Jimbo la Rombo Mhe. Prof Adolf Mkenda ambaye ni Waziri wa Kilimo akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano kwa vijana wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa vijana wa kata zote za Wilaya ya Rombo katika eneo la CCM Wilayani Rombo. (Picha na Mathias Canal)


Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Rombo umepongezwa kwa usimamizi madhubuti wa Uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Octoba 2020 na kukifanya Chama Cha Mapinduzi kuibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia nyingi.


Mbunge wa Jimbo la Rombo Mhe. Prof Adolf Mkenda ambaye ni Waziri wa Kilimo ametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa vijana wa kata zote za Wilaya ya Rombo katika eneo la CCM Wilayani Rombo.


Prof Mkenda amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM ni nguzo imara ya ushindi wa chama hicho kwani katika uchaguzi mkuu walisimamia maslahi ya chama hicho kilichotangazwa mshindi wa uchaguzi.


"Mimi sikuwa na hela za kuwalipa vijana kwa kazi kubwa mliyoifanya wakati wa uchaguzi lakini leo nimewaita kuwashukuru na kuonyesha jinsi nilivyotambua umuhimu wenu kwa namna mlivyojitoa kwa maslahi ya jumuiya na Chama kwa ujumla wake" Amesisitiza Prof Mkenda


Awali Mbunge Mkenda amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Jimbo la Rombo ambapo amekagua miradi ya maendeleo iliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025


Miradi hiyo aliyoikagua ni pamoja na ujenzi wa choo cha Shule ya Msingi Hakwe Kata ya Mamsera, mradi wa ujenzi wa choo kwenye bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Mahida Kata ya Mahida, na ujenzi wa choo cha walimu wa shule ya msingi Udangeni kata ya Chala.


Miradi mingine aliyoikagua ni Ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya msingi Horombo uliopo Kata ya Ngoyoni, na ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Kwamwera Kata ya Ushiri Ikuini.


Waziri Mkenda ameahidi kutuma mtaalamu wa kilimo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kilimo cha migomba katika shule ya Sekondari Mahida kwani shule hiyo ina mradi maalumu wa kilimo cha migomba.


Katika ziara hiyo mkoani Kilimanjaro Waziri Mkenda ametembelea na kukagua shughuli za ununuzi na uzalishaji wa miche bora ya kahawa katika chama cha msingi cha ushirika (USHIRI AMCOS) kilichopo Kata ya Ushiri ambapo amekipongeza chama hicho kwa ufanisi mkubwa wa uzalishaji miche bora wanaoufanya.


Akiwa katika ukaguzi wa miradi hiyo Mbunge Mkenda amewahakishia madiwani na viongozi wa vijiji kuwa serikali imejipanga imara kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati uliokusudiwa.


Amesema kuwa kwenye sekta ya elimu kama mbunge wa jimbo hilo la Rombo ataendelea kuhakikisha anaisimamia vyema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakisha changamoto zote katika sekta ya elimu zinatatuliwa kwa wakati.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana