Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI RWANDA KWA KUTEMBELEA VIWANDA VITATU, AREJEA DAR ES SALAAM, LEO

Na Mwandishi Maalum

Rais Samia Suluhu Hassan leo amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Rwanda kwa kutembelea viwanda vitatu na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na viwanda hivyo.


Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema, Rais Samia  akiwa na mwenyeki wake Rais Paul Kagame wa Rwanda alianza kutembelea Kiwanda cha Inyange kinachotengeneza vinywaji ambako aliona shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na maji ya kunywa, maziwa na juisi.


Rais Samia alitembelea pia Kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi cha Mara Phonena na kujionea hatua mbalimbali za utengenezaji wa simu kuanzia hatua ya awali hadi kukamilika kwake kisha akatembelea kiwanda cha uunganishaji magari cha Volkswagen kilichopo nchini humo na kujionea hatua mbalimbali za kuunganisha magari hayo ambayo huuzwa nchini humo. 


Taarifa imesema, baadaye Rais Samia aliwaagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji  Geoffrey Mwambe kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo alivyotembelea ili kutumia fursa zilizopo katika viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuwauzia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania.


Baaye Rais Samia aliagana na mwenyeji wake Rais Kagame katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali na kurejea Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa kupungiana mikono baada ya kupanda Ndege wenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali tayari kurejea jijini Dar es Salaam, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti, 2021.
Rais Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame na Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Reberatus Mulamula. 
Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha CFAO MOTORS kinachotengeneza Magari aina ya Vokswagen kuhusu huduma zinazotolewa wakati walipotembelea  kiwanda hicho leo tarehe  03 Agosti,2021.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana