Ikulu, Dar es Salaam, leo
Rais Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu Agosti 2, 2021 anatarajia kuondoka hapa nchini kwenda nchini Rwanda kufanya ziara ya Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.
Taarifa ikiliyolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Raais, Ikulu Jaffar Haniu, imesema Rais Samia pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Kagame, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa ziara hiyo ya siku mbili inalengakuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania.
Post a Comment