Prof. Apollinary Kamuhabwa akizungumza jambo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Donald Wright mara alipotembelea Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) jana Sept 13, 2021. Kwalengo la kutembelea miradi inayo fadhiliwa na Wamarekani.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Donald Wright (katikati) akizungumza jambo mara alipotembelea kitengo cha dharula cha Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga alisema idara hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa 200 hadi 300 kwa siku kutoka maeneo mbalimbali ya nchi pamoja na nje ya nchi.
Idara hiyo inatoa huduma za dharura pamoja na kufundisha wataalamu mbalimbali wanaotoa huduma za dharura nchini na nje ya nchi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili, Dkt. Jessie Mbwambo akizungumza jambo katika Mkutano uliohusisha Taasisi tatu za Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS, Hospitali ya Taifa Muhimbili MNH Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Ocean Road JKCI.
Balozi Wright amefanya ziara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ambako ameelezwa jinsi tafiti za kudhibiti magonjwa mbalimbali zilivyofanyika. Utafiti huo umejumuisha magonjwa ya afya ya akili, malaria, kifua kikuu, ajali na magonjwa yasioambukiza.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusino MUHAS Helen Mtui akizungumza jambo katika Mkutano huo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili, Dkt. Jessie
Mbwambo alimweleza balozi huyo jinsi
idara hiyo ilivyofanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa afya ya akili nchini, Katika Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, baadhi ya watu waliotibiwa kwa muda mrefu walitoa ushuhuda jinsi walivyopona na sasa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Prof. Mohamed Janabi akimuelekeza jambo Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Donald Wright mara walipofika katika chumba cha Upasuji ulipokuwa ukiendele ndani
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Prof. Mohamed Janabi (kulia) jambo Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Donald Wright mara walipofika katika chumba cha watoto
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment