Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakisherehekea wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya St Anne Marie Acdemy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akimlisha keki mmoja wa wazazi waliohudhuria mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wa kucheza michezo mbalimbali wakati wa mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
WAZAZI na walezi wamepongeza Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, dk. Jasson Rweikiza kwa uwekezaji kwenye elimu huku wakipongeza pia mafanikio ya shule ya St. Anne Marie Academy kwenye matokeo mbalimbali ya mitihani ya kitaifa na kuwataka walimu wasibweteke.
Walitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafai ya 17 ya kidato cha nne, yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi hao, Anitha Umbula alisema wazazi wamefurahia maendeleo mazuri ya kitaaluma ya shule hiyo na mazingira mazuri ya shule hiyo huku akiwataka walimu wasibweteke.
Anitha alisema kwa miaka karibu saba mfululizo shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuingia kwenye kumi bora kitaifa na kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ubungo.
“Haya si mafanikio madogo ni makubwa sana lazima tuwapongeze walimu na Dk. Rweikiza kwa uwekezaji mkubwa mnaoufanya kwenye shule hii lakini msibweteke kwa mafanikio haya,” alisema
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza aliomba wazazi waendelee kuiamini shule hiyo.
Alisema wamekuwa wakifanya maboresho makubwa kila mwaka lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanaopitia shule hiyo wanapata matokeo mazuri kitaifa.
Alisema wana maktaba zilizosheheni vitabu ikiwa na kiyoyozi, maabara zenye vifaa kwaajili ya sayansi kwa vitendo, kitengo cha udhibiti ubora cha ndani na bodi ya mitihani inayoratibu mitihani ya ndani ya shule.
Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabula alisema kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2017, wanafunzo wote 43 wastani wa alama A na kuwa ya kwanza Wilaya ya Ubungo, ya pili Mkoa wa Dar es Salaam na ya nane kitaifa.
Alisema mwaka 2018 wanafunzi wote 59 walipata alama A na shule kuwa ya kwanza Wilaya ya Ubungo, ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam nay a sita kitaifa.
Ndiyetabura alisema kwenye matokeo ya kitaifa mwaka 2019 wanafunzi wote 99 walipata wastani wa alama A, shule kuwa ya kwanza Wilaya ya Ubungo, ya kwanza Mkoa wa Dar es salaam na ya13 kitaifa.
Kwa mwaka 2020, Ndyetabura alisema wanafunzi wote 129 walipata alama A, ikawa ya kwanza Wilaya ya Ubungo, ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na ya nane kitaifa.
Post a Comment