Mratibu wa Tamasha hilo, Debora Malassy akiomba wakati wa kikao hicho kilichofanyika Chuo cha Ufundi VETA Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mkesha huo.
Ilikuwa ni kuimba na kumuabudu Mungu wakati wa kikao hicho cha maandalizi.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MAANDALIZI ya Mkesha mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa na viongozi ili Tanzania iwe ya amani na utulivu litakalofanyika Desemba 31 yameanza.
Maandalizi hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Tamasha hilo la Dua Maalumu kwa Taifa, Askofu Godfrey Malassy amesema katika kikao cha maandalizi , kuwa mkesha huo utafanyika tarehe hiyo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Tamasha hilo lililoanyishwa 2009 Kwa Dodoma litakuwa la 8.
Ametoa rai kwa wananchi bila kujali itikadi ya dini wala vyama kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwa kushiriki kuomba na kuwa shahidi wa matendo makuu, juu ya Taifa la Tanzania kuwa la amani na utulivu.
Sote tunafahamu Taifa letu limekuwepo miaka yote na limekuwepo na amani ya kudumu lakini watu wengi hawajui siri yake ni nini? Nchi nyingi duniani leo wanauliza Tanzania kuna nini inakuwaje inakuwa na amani ya kudumu? wakati majirani zetu hakuishi kukucha ni vita?
Si kwamba Tanzania na majeshi imara, wananchi, lakini hiyo si sababu, nchi nyingine pia zina majeshi lakini ni vita asubuhi na jioni. Nitawambia siri hiyo, ni kwamba Tanzania imechorwa kwenye kiganja cha Mungu, Tanzania imewekwa katika moja ya majukumu ya siku ya mwisho.
Ili kuthibitisha maneno hayo , Askofu Malassy amewaomba watanzania kusoma neno la Mungu kwenye Biblia kwa kufunua Sura 18 mstari wa 1-7 ambayo inaeleza nchi ambayo ilipandisha bendera mlimani na kwamba utabiri huu ulitokea miaka 600 kabla ya kuzaliwa Kristo. Wakati wa Uhuru 1961 Tanzania ilipandisha Bendera ya Taifa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Amesema kwa uthibitisho huo Tanzania ni nchi ya kipekee ulimwenguni hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuliombea taifa , Rais na Serikali ili wanapokuwa wanatawala watawale kwa kichwa cha Mungu ili amani na utulivu uendelee
Askofu Malassy amesema pia kuwa madhumuni mengine ya mkesha huo ni kuomba kuhakikisha Mungu anaiponya Tanzania na ugonjwa wa Corona, kama alivyoliponya huko nyuma ambapo pia aliwataka watanzania kuchukua tahadhari nyingine zaidi.
Kikao hicho cha maandalizi kilihudhuriwa pia na viongozi wengine wa kamati ya maandalizi ambao ni, Juliana Manyerere, Mchungaji Rose Amani, Rose Massawe na Debora Malassy na wengineo.
Post a Comment