Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki za NMB, Filbert Mponzi akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa Bunge Sports, Abbas Tarimba kwa ajili ya Tamasha la Michezo kati ya NMB na Bunge Sports litakalofanyika Septemba 4 kwenye Uwanja wa Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma. Aliyeshika jezi kulia ni Makamu Mwenzekiti wa Bunge Sports, Ester Matiku.
Nmb imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 12 vitakavyotumika kwenye michezo 7 itakayohusishwa siku hiyo ambayo ni. mpira wa miguu, basketi wanawake na wanaume, mpira wa wavu, netiboli, kuvuta kamba, na kukimbiza kuku.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Kivumbi na Jasho ambalo pia ni sehemu za maandalizi ya mbio za NMB Marathon 2021 (Mwendo wa Upendo) litakalofanyika Septemba 18, 2021 jijini Dar es Salaam, litaanza kwa mbio ya taratibu (Jogging) kutoka viwanja vya Bunge hadi Uwanja wa Jamhuri.
Mponyi akikabidhi moja za mipira itakayotumika siku hiyo.
Mponyi, Taimba na Matiku wakiwa wameshima baadhi zya mipira hiyo.
Wakionesha jezi na vifaa vingine vya michezo
Tarimba na Matiku wakiteta kuweka mambo sawa.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment