Featured

    Featured Posts

VIONGOZI 120 WA TGGA WAPIGWA MSASA UMUHIMU WA RASILIMALI FEDHA

Viongozi wa Chama cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA),  wakisiliza kwa makini wakati Mkufunzi na Mshauri wa Mambo ya Sheria wa chama hicho, Maria Richard, akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa Rasilimali Fedha katika kuendesha Taasisi hiyo, wakati wa Kambi ya Mafunzo Elekezi  kwa Viongozi  wa  Taasisi hiyo kutoka mikoa 20 ya Bara na Visiwani.

Mkufunzi na Mshauri wa Mambo ya Sheria wa Chama cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA),  Maria Richard, akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa Rasilimali Fedha katika kuendesha Taasisi hiyo, wakati wa Kambi ya Mafunzo Elekezi  kwa Viongozi  wa  Taasisi hiyo kutoka mikoa 20 ya Bara na Visiwani.

Mafunzo hayo ya siku 6 yamefunguliwa jana na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA,  Anna Maembe katika Shule ya Sekondari ya Fundi Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Maria Richard  ametoa Mafunzo kuhusu, jinsi ya kuongeza mapato, Mahusiano ya Serikali, asasi mbalimbali na wao  kwa wao,ujasiriamali. Ada za uanachama, Kanuni za Fedha  na Utawala TGGA, mchango wa Thinking Day na jinsi ya kufanya manunuzi na marejesho (retirement).
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi akielezea umuhimu wa kiongozi kuandaa mapema  viongozi wa kurithi nafasi aliyonayo atakapostaafu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Anna Maembe akitoa mada kuhusu kiongozi bora anavyotakiwa kuwa.
Kamishna wa Kimataifa, Shahyeen Rashid akielezea kuhusu Sera ya Mafunzo ya WAGGGS.
Mwenzekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro akitoa mafunzo ya jinsi ya kujitia moyo na kujiamini katika jambo lolote unalolifanya.
Mwenyekiti wa TGGA Zanzibar, Sauda Pandu Amour akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.
Mwanamani Evarist kiongozi wa Vijana wa TGGA  Kilimanjaro akijibu swali za jinsi alivzoelewa kuhusu uongozi.
Washiriki wakifanya mafunzo kwa njia ya makundi.


Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi (kushoto) akijadliana jambo na Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Qorro.





Viongozi wa TGGA wakisikiliza kwa makini kuhusu mada hiyo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliya/kuona kupitia clip hii ya video Mkufunzo Maria Richard akitoa mafunzo kuhusu rasilimali fedha na viongozi wakielezea jinsi walivyoelewa .......

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana