Na CCM Blog. Tegeta
Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, limekuwa likiendesha Ibada zake mara kwa mara hususan siku za Jumapili, na ibada hizo zote huonyesha kuwa zimeacha alama bora na imarata kwa waaumini wake ambao kulingana na Kanisa hilo wanafamika kwa jina la Uzao Halisi.
Ibada zilizo kubwa huendeshwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo anayetambulika kwa jina la Baba Halisi wa Uzao.
Katika Ibada ambazo zimewahi kushuhudiwa na Mwandishi wa habari hii, japo zote zimekuwa na mada motomoto kutoka kwa Baba Halisi wa Uzao, Ibada iliyofaanyika Jumapili ya Oktoba 10, 2021 (26 Abu Vol.2) naweza kuandika kuwa ilikuwa ya kipekee mno.
Ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na Uzao pomoni, ilikuwa ya aina yake kwa kuwa, mada yake ilikuwa inahusu zaidi jamii kwa kuwa ililenga kuwafunda Waumini wa Kanisa hilo na wananchi kwa jumla kwamba, wanapaswa kujua kuwa Ibada iliyo njema na sahihi mbele za Mungu ni kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi kwa Bidii, juhudi, maarifa na uadilifu.
Katika ibada hiyo ambayo ilitwa ' Ibada ya Mauzo na Uzalishaji' iliambatana na maonyesho ya huduma na bidhaa mbalimbali za Wazalishaji.
Akizindua rasmi Ibada hiyo, Baba Halisi alifafanua kwa kina akirejea katika Biblia kwamba mtu akifanya kazi yoyote halali na akaitenda kwa uaminifu basi hiyo ndiyo ibada yenyewe.
"Ukiendesha Bodaboda, ukawatendea haki abiria wako, au Mama lishe akawatendea haki wateja wake hiyo ndiyo ibada. hata ukiwa mtoa huduma kwenye ofisi ukiwatendea haki wateja bila kuomba rushwa au kuonyesha dharau kwa kuangalia umhuduie kwanza nani umbague hiyo ndiyo Ibada.
Hata Mwandishi wa habari, akiandika habari zake kwa uadilifu ni ibada, hata mwanafunzi akisoma masomo kwa bidii, juhudi na maarifa na akawa mwadilifu katika usomaji wake hiyo pia ni ibada, hata viongozi wa duni, akiongoza vizuri nayo ni kazi hiyo wakiitenda kwa uadilifu ndiyo ibada yenyewe", alisisitiza Baba Halisi wa Uzao na kuendelea kutoka mifano mbalimbali kudhuhirisha kuwa Kazi yoyote halali ikifanywa kwa uadilifu ndiyo ibada yenyewe.
Baba Halisi amesema, kutokana na umuhimu, Kanisa hilo litakuwa linaifanya ibada hiyo ya Uzalishaji mali hadi pale jamii itakapoelewa kuwa ibada ni uzalishaji na sio kulia na kuomboleza tu kwenye nyumba za ibada.
"Tulipoanza ibada katika 'level' ya unabii maswali yalikuwa mengi, mbona Yesu alipindua meza za wafanyabishara hekaluni. Nisikilizeni kwa makini, Yesu alipopindua meza hizo hakumaanisha kukataa uzalishaji bali wapangaji wabaya ikiwemo uzinzi, uasherati, wivu, chuki na kiburi vitoke mioyoni." Amesema.
Aidha ameitaka jamii kufanya kila kitu kwa utii na haki wakiwemo wanafunzi kwa kusoma kwa bidii na utii, madaktari kutoa huduma kwa haki na madereva kuendesha vizuri na kwa halali na kwa kufanya hivyo ni ibada.
Kanisa Halisi la Baba Mungu ambalo lilianzishwa mwaka 1984 lina vituo nchi nzima na mataifa 136 na limejijenga katika misingi ya imani, amani, upendo, matendo mema na ibada hiyo ya uzalishaji mali.
Katika Ibada hiyo Kanisa liliwakutanisha watoa huduma, wazalishaji na wafanyabishara mbalimbali kwa ajili ya kuuza na kutangaza bidhaa zao ambapo miongoni waliohudhuria ni Kina mama wajasiriamali watano kutoka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Kunduchi.
Kina mama hao ambao baadhi yao walipata mikopo isiyo na riba ambayo hutolewa na Serikali kupitia Halmashauri zote nchini waliweza kupewa na Kanisa hilo nafsi za kuonyesha bidhaa zao bila kutoa gharama yoyote.
Post a Comment