Magazeti ya leo, gazeti la mwananchi, global publisher, habari leo, habari mpya, ippmedia,magazeti ya leo tanzania, magazeti ya udaku, michuzi, michuzi blog, mpekuzi huru, mwananchi, mwanaspoti,nipashe, sekretarieti ya ajira
Mchezaji wa timu ya Unguja wanawake akijitahidi kumpita mchezaji wa timu ya Mkoa wa Tanga katika mchezo wa nusu fainali ya mpira wa kikapu ya CRDB BANK Taifa Cup kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma Novemba 13,2021.
Kilele cha mashindano hayo ambayo mdhamini mkuu ni Benki ya CRDB, kinafanyika leo ambapo kwa upande wa wanaume timu zilizoingia fainali ni Dar es Salaam na Arusha na Wanawake ni Dar es Salaam na Unguja. Fainali ya wanawake inaanza saa 11 jioni na upande wa wanaume watapepetana kuanzia saa 1 usiku.
Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi.
Wapenzi wa mchezo huo wakishuhudia pambano kati ya Unguja na Tanga wanawake.
Mtanange ukiendelea
Wachezaji wa timu ya Unguja wakishangilia kiaina baada kufuzu fainali kwa kuibwaga timu ya Mkoa wa Tanga katika mchezo wa nusu fainali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela (wa pili kushoto waliokaa meza kuu) akishuhudia pambano la mpira wa kikapu wanawake kati ya Unguja na mkoa wa Tanga. Unguja walishinda na kuingia fainali.
Nsekela akisalimiana na mmoja wa wapenzi wa mpira wa kikapu.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kuona mpambano wa nusu fainali Unguja na Tanga...
Post a Comment