Iramba, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda wiki hii akiwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Lemomo Ole Kiruswa wametembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu na kuzungumza na wachimbanji wadogo wa ushirika wa Ukombozi katika Kijiji cha Nkonkilangi Tarafa ya Shelui Wilayani humo na kueleza mipango mikubwa ya uongozi wa Wilaya hiyo katika kuiimarisha sekta hiyo muhimu kwenye mapato ya Wilaya ya Iramba na nchi kwa ujumla.
Mgodi huo kwa mwaka hutoa zaidi ya gram Laki 3 na elfu 19 za dhahabu na kuiingizia Serikali Bilioni 37 huku Wilaya ikiingiza mapato ya zaidi ya Milioni 460. Mpango wa Serikali ya Wilaya ya Iramba inayosimamiwa na Mhe Mwenda ni kuhakikisha uzalishaji unakuwa kufikia gramu Laki 6 ambazo zitaiingizia Serikali kiasi cha Bilioni 80 pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya kwa zaidi ya Bilioni 1.
Zaidi ya asilimia 9 ya mapato yatokanayo na madini ambayo Taifa linaingiza, hutokea kwenye mgodi huo uliopo Wilayani Iramba.
Post a Comment