Akizungumza jana Januari 7, Shahidi wa 13 ambaye ni Ofisa Uchunguzi kutoka Taasisi ya Kupamana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Ramadhan Juma ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa, Sabaya alijitambilisha kama Mkuu wa kikosi kazi maalum cha kupambana na uhujumu uchumi Kanda ya Kaskazini.
Alisema Sabaya alitumia cheo alipofika gereji ya mfanyabiashara Francis Mrosso, akidai kuwa cheo hicho alipewa na Rais Magufuli.
SOMA: Ofisa Takukuru aeleza uhusika watuhumiwa kesi ya Sabaya
Akihojiwa na Wakili wa utetezi, Sylvester Kahunduka, mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa walipomkamata Sabaya na wenzake jijini Dar es Salaam, walimkamata na fedha ambazo ni mazalia ya rushwa katika tuhuma zingine zinazomkabili.
Post a Comment