Afisa Maendeleo ya Vijana Mwandamizi Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale (kushoto) amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kikimpa ridhaa ya kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anaimarisha mahusiano na mihimili mingine ambayo ni Serikali na Mahakama pamoja na kumshauri Rais kwa hekima na busara. Mwasamale ambaye pia amewahi kuwa mmoja wa waratibu wa Bunge Maalumu la Katiba ameyasema hayo baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea Uspika wa Bunge hilo katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma Leo. Anayepokea fomu hizo ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomoni Itunda.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mwasamale akielezea kilichomsukuma kuwania Uspika.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment