Vitabu vikiwa vimepangwa katika maktaba hiyo.
Jango la Maktaba hiyo.
Wananvijiji wamekuwa wakichangia nguvu kazi na fedha taslimu kujenga Maktaba na Maabara katika shule Jimbo la Musoma Vijijini.
Hamasa hiyo ya wananchi kuwa na moyo wa kujitolea imekuwa ikitolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo ambaye amekuwa mstari wa mbele kuchangia kwa hali na mali pamoja na fedha kukamilisha ujenzi huo.
Wanafunzi na wanavijiji wametoa pongezi kwa mbunge wao huyo na shirika binafsi la PCI Tanzania kwa michango mikubwa waliyotoa kukamilisha ujenzi huo pamoja na kutoa msaada wa vitabu katika maktaba.
MAKTABA ya Shule ya Msingi Karubugu, Kijijini Kurwaki IMEKAMILIKA na tayari imeanza kutumika.
*Wanakijiji wamechangia nguvukazi na fedha taslimu. Daftari linaloonyesha MICHANGO iliyotolewa liko kwenye Serikali ya Kijiji cha Kurwaki.
*WANAFUNZI na WAKAZI wengine wa Vijiji vya Kurwaki na Kiriba, na Viongozi wa Kata zao WANAISHUKURU sana PCI TANZANIA na MBUNGE wao wa Jimbo Prof Muhongo kwa KUTOA MICHANGO MIKUBWA kukamilisha UJENZI wa MAKTABA ya Shule yao ya Msingi.
Wanafunzi wa S/M Karubugu wanatoka Vijiji vya Kurwaki (Kata ya Mugango) na Kiriba (Kata ya Kiriba)
MATUMIZI ya MAKTABA ILIYOJENGWA & KUKAMILIKA
*Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanakaribishwa
*Walimu wa shule za Msingi na Sekondari wanakaribishwa.
*Wakazi wa Vijiji na Kata za jirani wanakaribishwa.
UJENZI WA MAKTABA NA MAABARA ZA SAYANSI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI UNAENDELEA.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or tz
Post a Comment