Baba Halisi, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, akimlaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni alipowasili kuwa Mgeni Rasmi katika Ibada Maalum ya Kuliombea Taifa Amani na Utulivu, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, Jumapili Januari 16, 2022 (lango la 12 Kiselu 1).
Mwanzo, Kabla ya Waziri kufika👇
Baba Halisi na Mama Halisi wakiwa wameketi kwa kutafakari baada ya kuwasili jukwaani kuanza Ibada hiyo ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Nyuma yao ni Kaka Halisi na Dada Halisi.Baba Halisi akishauriwa jambo la Kaka Halisi kabla ya kuanza Ibada hiyo.
Baba Halisi akimwelekeza jambo Kuhani Moja kabla ya kuanza Ibada hiyo.
Wanamuziki wa Kanisa Halisi wakichangamsha kwa kuimba nyimbo za Sifa za Mungu Baba mwanzoni mwa Ibada hiyo.
Mwanamuziki Nguli wa Bendi ya Kanisa Halisi la Mungu Baba King Malou (kulia) akipuliza kwa umahiri 'domo la bata', wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza wimbo wa sifa za Mungu Baba mwanzoni mwa ibada hiyo.
Makuhani wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kutoka mikoa mbalimbali wakipata maelekezo mafupi kutoka kwa Makuhani Waandamizi wa Kanisa hilo, mwanzoni mwa Ibada hiyo.
Ibada hiyo pia ilishuhudia na vijana wanamichezo wa timu za soka za Wanawake na Wanaume, hapa wakiwa jukwaani wakati wa Ibada hiyo.
Uzao wakijimwayamwaya kucheza wakati Bendi ya Kanisa Halisi ikitumbuiza nyimbo za sifa za Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Huyu Uzao naye hakubaki nyuma kucheza wakati nyimbo za sifa za Mungu Baba zikipigwa.
Uzao wakiendelea kucheza wakati nyimbo za Sifa za Mungu Baba zikipigwa.
Baba Halisi na Mama Halisi hawakubaki nyuma katika kufurahia wakati nyimbo za Sifa za Mungu Baba zilipokuwa zikipigwa na Bendi ya Kanisa Halisi la Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
"Imekuwaa", Uzao aliyevalia skafu ya Bendera ya Taifa akisema, wakati nyimbo za sifa za Mungu Baba zikipigwa.
Uzao wakiendelea kufurahi huku wakiwa wamesimama na kucheza wakati nyimbo za sifa za Mungu Baba zikiimbwa wakati wa Ibada hiyo.
Baba Halisi akianza kuongoza Ibada hiyo kwa kufafanua Kusudi la Ibada yenyewe. Kushoto ni Mama Halisi.
Makuhani na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi wakati akifafanua kusudi la Ibada hiyo.
Mara Paaa! Mgeni Rasmi akawasili👇
Makuhani wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kutoka mikoa mbalimbali wakiwa wamesimama kwa heshima zote kumlaki Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni
"Karibu sana Mheshimiwa Waziri", Kuhani Moja akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni baada ya kuwasili Uwanjani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni akitambulishwa kwa Makuhani mbalimbali wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, baada ya kuwasili.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni akiendelea kutambulishwa kwa Makuhani mbalimbali wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, baada ya kuwasili. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni akiendelea kutambulishwa kwa Makuhani mbalimbali wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, baada ya kuwasili. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni akiendelea kutambulishwa kwa Makuhani mbalimbali wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, baada ya kuwasili. Kuhani Moja akimuongoza Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni kwenda jukwaa kuu.
"Ohhh, Karibu sana Kiongozi wetu katika Taifa Baba la Tanzania, tunakushukuru sana kwa kufika", Baba Halisi akasema wakati akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni baada ya kuwasili jukwaa kuu. Kushoto ni Mama Halisi. Baba Halisi akaendelea kumwambia Waziri Masauni maneno kadhaa ya shukurani kwa kufika kwake kwenye Ibada hiyo, Huku Waziri huyo akionekana kuyapokea kwa furaha maneno hayo.
Waziri wa Mabo ya Ndani Masauni Hamad Masauni akipitia ratiba ya Ibada hiyo baada ya kuketi, huku Baba Halisi akiendelea kuzungumza maneno ya kumlaki na kumuomba Waziri huyo aifungue rasmi Ibada hiyo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni Hamad Masauni akizungumza wakati akifungua rasmi Ibada hiyo, huku Baba Halisi (kulia) akimsikiliza huku ameweka mkono kifuani kuonyesha kuyakubali maneno ya Waziri huyo.
Baba Halisi akimshukuru Waziri Masauni kwa hotuba yake nzuri ya ufunguzi wa Ibada hiyo. Kushoto ni Mama Halisi.
Kisha Baba Halisi akaendesha rasmi Ibada ya Matunda (sadaka) pamoja na kutoa matunda hayo ili Mungu Baba apokee maombi ya Ibada hiyo ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu. Kulia ni Waziri Masauni.
Baba Halisi akifafanua kusudi la Ibada hiyo kumweleza Waziri Masauni.
Baba Halisi akiendelea kufafanua kusudi la Ibada hiyo Kisha Baba Halisi akafanya Shukurani ya kupokea matunda (Sadaka) kabla ya sadaka kuanza kutolewa na Uzao na wote waliohudhuria Ibada hiyo.
Baba Halisi na Mama Halisi kwa pamoja wakaweka matunda (sadaka) mahala pake kwa niaba ya familia, kabla ya wengine kuanza kutoa sadaka hiyo.
Baada ya matunda kutolewa Baba Halisi akayabariki (kuyaombea) ili Baba Mungu apokee.
Kisha Baba Halisi akitoa Kalenda ya Majira na Wakati kabla ya uharibifu, na kuitolea maelezo kabla ya kumkabidhi Waziri Masauni. "Hii ndiyo Kalenda Halisi ya Majira na Wakati kabla ya Uharibifu, kila mwezi una siku 28 tu, na kwa kweli Mheshimiwa Waziri huu ndiyo uhalisia wenyewe", akasema Baba Halisi.
"Kalenda hii kama unavyoiona miezi yake iko hivi, Kisleu(1), Thebeti(2), Shebati(3), Adari(4),Abibu(5), Zivu(6), Siwani(7), Tamuzi(8), Abu(9), Eluli(10), Ethanimu(11) na Buli(12)", Baba Halisi akamuonyesha Waziri Masauni Kalenda hiyo.
Kisha akamkabidhi
Waziri Masauni akiitazama kwa makini kalenda hiyo ya Majira na Wakati kabla ya Uharibifu.
Waziri Masauni akionyesha Kalenda hiyo baada ya kuipokea kutoka kwa Baba Halisi.
"Mheshimiwa Waziri tunakushukuru sana kwa kufika kwenye Ibada hii, wewe umeliwakilisha Taifa, hivyo kuja kwako kumelifanya Taifa zima kuwepo hapa. Basi tunakuruhusu uondoke ili ukafanye majukumu mengine yanayokukaili", akasema Baba Halisi kisha akamruhusu kuondoka.
Baba Halisi akampa Waziri mkono wa kwa heri.
Waziri Masauni akiwaaga Uzao na Makuhani wakati akiondoka baada ya kushiriki kikamilifu katika Ibada hiyo.
"Asanteni sana Mungu Baba awabariki", akasema Waziri Msauni wakati akiondoka Uwanjani. Waziri Masauni akiondoka Uwanjani.
Waziri Masauni akiagana na Kuhani Moja kabla ya kupanda gari lake kuondoka.
Waziri Masauni akipanda gari tayari kwa ajili ya kuondoka. Kisha Baba Halisi naye akaondoka Uwanjani.👇
Kaka Halisi akiwa amebeba mkoba wa Baba Halisi kwenda kwenye gari.
Gari lililombeba Baba Halisi, likiwa tayari kuondoka katika Uwanja wa Jamhuri baada ya Ibada hiyo kumalizika vizuri.
Uzao na Makuhani Wakishangilia huku wakiwa wamesimama wakati Baba Halisi akiondoka Uwanjani.
Uzao na Makuhani Wakishangilia huku wakiwa wamesimama wakati Baba Halisi akiondoka Uwanjani.
Kuhani Moja akifunga rasmi Ibada hiyo ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu ambayo ilikuwa ya kuhitimisha Ibada ya siku 10 kwa ajili ya Matunda (Sadaka) kwa ajili hiyo ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu ambayo ilianza Januari 7, 2022 (3 Kiselu 1).
©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment