Featured

    Featured Posts

MATEMBEZI YA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR YATIKISA VIUNGA VYA ZANZIBAR

 









Baraza la Vijana Zanzibar likiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza Ndugu Yunus Juma Ali leo tarehe 26 Feb. 2022 wamezindua rasmi VIJANA Jogging Club. 

Uzinduzi huo wa aina yake umeshereheshwa na matembezi ya Kilomita 10 kuanzia Mapinduzi Square na kumalizikia Uwanja wa Mao Zedong ambapo walifanya mazoezi mbalimbali ya viungo huku viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi, Vyama vya siasa na vijana zaidi 200 wakijitokeza kushiriki mazoezi hayo. 

Akizungumza na umati wa Vijana waliojitokeza katika Uzinduzi huo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Yunus Juma Ali amesema "Tumezundua matembezi haya ya yenye lengo la kufanya mazoezi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Mariam Mwinyi alipokuwa anazindua Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation aliitaka jamii kumuunga mkono kwa kutoka kufanya mazoezi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na sisi kama Vijana tumesikia na leo ikiwa ni Jumamosi ya kwanza tangu atoe kauli ile tumeitekeleza kwa kishindo na tutafanya hivi kwenye maeneo yetu mbalimbali tunayoishi kila ifikapo Jumamosi ya mwisho wa mwezi. 

Mwenyekiti huyo wa Baraza alitumia nafasi hiyo kutoa maagizo kwa wenyeviti wote wa wilaya wa Baraza la Vijana Zanzibar kufanya hivyo kwenye maeneo yao kila ifikapo jumamosi ya mwisho. 

Pia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar alitumia fursa hiyo kuwahimiza vijana kujitokeza kushiriki zoezi la sensa pindi litakapoanza. 

Nae Mjumbe wa Kamati Tendaji Baraza la Vijana Zanzibar Amina Miraji ambae pia ni Katibu wa kamati ya Afya, Mazingira na Watu wenye Mahitaji Maalum amewataka Vijana kuendelea kujitokeza kufanya mazoezi kwani mazoezi ni Afya na amewasihi kufanya usafi kwenye maeneo yao kwani mazoezi na usafi uenda pamoja 

Aidha Vijana mbalimbali wamepongeza hatua hiyo ya kuzindua matembezi hayo kwa Vijana huku wakiahidi kufanya mazoezi kwenye maeneo yao
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana