Featured

    Featured Posts

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWAHAKIKISHIA WAKULIMA KUENDELEA KULINDWA NA SERIKALI DHIDI YA WANUNUZI WA MAZAO WABABAISHAJI

Na Mwandishi Maalum
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, amewahakikishia wakulima wote nchini kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuwalinda na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wafanyabiashara wa mazao ambao wanachukua mazao ya kulima na kushindwa kuwalipa.

Amesema Serikali itaendelea kuwalinda wakulima wote dhidi ya Wafanyabiashara hao kwa kuwa inatambua kuwa kuchukua mazao ya wakulima na kushindwa kuwalipa ni kitendo ambacho kinarudisha nyuma jitihada za kuinua sekta ya kilimo nchini na kupunguza umaskini kwa wananchi.

Mavunde ameyasema hayo kwa nyakati tofauti leo akijibu malalamiko ya wakulima juu ya walanguzi wa mazao katika wilaya za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi akiwa katika ziara ya siku tano kukagua shughuli zilizotekelezwa na Shirika Shirika la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA).

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mavunde amefuatana na Mjumbe wa Bodi ya  Shirika hilo Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais wa AGRA Aggy Konde.

“Wakulima wanatumia nguvu, rasilimali na muda wao mwingi kufanya uzalishaji kwa malengo ya kujiinua kiuchumi na kupunguza umaskini, hivyo Serikali haitaruhusu kamwe mtu yeyote kuwafanya wakulima kama mgongo wa kujiipatia mapato na kuwaacha wakitaabika kwa umaskini.

Tutahakikisha wanunuzi wa mazao ya wakulima wanawalipa kwa wakati wakulima kutokana na mauzo ya mazao yao, tutaendelea kuwabana na kuwashugulikia wale wote ambao wanaonesha ubabaishaji na kujaribu kufifisha jitihada za serikali katika kumuinua mkulima na kukuza sekta ya kilimo nchini", alisema Naibu Mavunde na kuongeza;

"Kile alichokifanya Waziri Hussein Bashe kwa wanunuzi wa Tumbaku waliochelewesha malipo ya wakulima ndio utakuwa muelekeo wetu kama Wizara katika kuwalinda wakulima”.

AGRA kwa kushirikiana na Serikali imesaidia ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao, kuwawezesha wazalishaji wa mbegu bora, kuwawezesha wachakataji wa mazao ya kilimo na kuwajengea uwezo wakulima kwa kuwalipia mafunzo juu ya kanuni za kilimo bora.

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza na Wakulima na Wananchi kwa jumla katika moja ya eneo ambalo yeye na ujumbe wake walifika wakiwa katika ziara hiyo mkoani Sumbawanga. Ujumbe aliofuatana nao ni pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Shirika Shirika la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA) Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais wa AGRA Aggy Konde.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika Shirika la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA) Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Wakulima na Wananchi katika moja ya mashamba ya mahindi, alipofia yeye na Naibu Waziri Mavunde wakiwa katika ziara hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika Shirika la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA) Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akitazama zao la mhindi kama lina ustawi unaostahili, katika moja ya mashamba ya zao hilo, ambalo walitembelea.
Naibu Waziri Mavunde, Mjumbe wa Bodi ya (AGRA) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais wa AGRA Aggy Konde, wakisikilizwa na Wakulima na Wananchi katika moja ya eneo walilofanya mkutano wakiwa katika ziara hiyo.
Naibu Waziri Mavunde (aliyeipa mgongo Kamera) akizungumza na wakulima na wananchi kwa jumla katika mkutano uliofanyika kwenye moja ya maeneo aliyofika akiwa katika ziara hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya (AGRA) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akizungumza jambo alipotembelea moja ya mashamba ya wakulima katika ziara hiyo.
Naibu Waziri Mavunde akizungumza na wakulima na wananchi.
"Kwa hiyo hii mashine inawasaidia vizuri?", Mjumbe wa Bodi ya (AGRA) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiuliza wakati akiwa katika moja na maghala ya kuhifadhi mahidi, wakati wa ziara hiyo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Mavunde. (Picha zote na Wizara ya Kilimo).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana