Featured

    Featured Posts

HIJA YA KANISA HALISI ILIVYOTIKISA KIGOMA, MAHUJAJI WAFURIKA UWANJA WA LAKE TANGANYIKA, BABA HALISI AMWINUA RAIS SAMIA KABLA YA KUACHIA BARAKA

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi ya Mungu Baba, lenye Makao yake Makuu Tegeta Jijini Dar es Salaam, Baba Halisi akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Alexender Mahawe baada ya hotuba aliyoitoa Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua Ibada ya Hija ya Chanzo Halisi, iliyofanyika juzi, Jumapili ya Februari 27, 2022, (26 Thebeti Majira Halisi), katika Uwanja wa Lake Tanganyika,

Na CCM Blog, Kigoma.
Ibada ya Hija ya Chanzo Halisi iliyofanyika
juzi, Jumapili ya Februari 27, 2022, (26 Thebeti Majira Halisi), katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma ilifanikiwa kuutikisha mkoa huo, kwa kufurika Mahujaji kutoka mikoa yote nchini na Nchi za Nje.

Mbali na Mahujaji ambao walitoka mikoa yote nchini na wengine nchi za nje zikiwemo Marekani, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zambia pia ibada hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, Masheikh, Mapadre na Wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali wakiwemo Wakatoliki.

Ibada hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Alexernder Mahawe akimwakilisha Mkuu wa mkoa huo Thobias Andengenye, kabla ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi kuachia Baraka zilizokusudiwa kupatikana kwenye Hija hiyo, alitanguliza kumwinua (kumuombea) Rais Samia Suluhu Hassan.

"Heri, Heri.  Kama mnavyoona Mwenyeji wetu ambaye ni Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, akimwakilisha Mkuu wa mkoa huu ameshafika mahala hapa, maana yake ni kwamba Kigoma yote ipo hapa, lakini kabla sijaachia Baraka kwa wote mliopo hapa na msiokuwepo, kwanza nitamwinua (kumuombea) Kiongozi wa Nchi yetu Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake.

Hii tufanya ikiwa ni wajibu wetu kwa kuwa Mungu Baba ametuagiza kuwainua viongozi wa nchi kwenye Ibada zetu, hiyo tunamwinua Rais Samia ili aendelee kuwa na afya njema, na kujawa na hekima na busara ili aweze kulitumikia taifa letu vyema", alisema Baba Halisi na kumumba Mkuu wa Wilaya na Kaimu DAS Maximilian Ngasa kusimama mbele yake.

Baada ya Mahujaji ambao ni Uzao wa Kanisa Halisi, na waliohudhuria wote kusimama, Baba Halisi alianza kuendesha Shukurani hiyo ya Kumuinua Rais Samia na baada ya kumaliza akasema " Sasa tumeshamwinua Mkuu wa Nchi yetu na wote waliopo chini yake, kwa hiyo naanza kuachia Baraka kwa kila aliyehudhuria hapa na ambaye hayupo mahala hapa.

Lakini kabla ya hapo naomba niseme kuwa kila ambaye aliwahi kunitukana hata bila mimi mwenye kujua, nasema namsamehe bure, hivyo nitaachia baraka kwa kila mmoja, na ambaye hazitamfika basi litakuwa ni tatizo lake mwenyewe, maana woote waliowahi kunitukana au nikosea kwa lolote nimewasawamehe bure kabisa".

Baada ya kauli niyo, Baba Halisi alianza kufanya shukurani ya kuachia Baraka kwa kila mtu.

Mapema akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Baba Halisi alimweleza kuwa Kanisa Halisi ni Kanisa ambayo limejipambanua katika mambo makuu matatu aliyoyataja kuwa ni Amani, Upendo usiobagua na Uzalishaji

Baba Halisi alifafanua kwamba Hija ya Kigoma siyo hija ya watu kwenda kutazama kumbukumbu, bali ni Hija Halisi ya kwenda kupokea Baraka, kisha akafafanua pia kwa nini Hija inafanwa na Kanisa Halisi mkoani Kigoma na siyo mkoa mwingine wowote au kwingineko Duniani.

"Mwaka 2019 Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu) ilisikika Kigoma,

Sasa Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri. Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri. Hija hii ya Chanzo Halisi cha Mungu Baba tunayofanya hapa mjini Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi", alisema Baba Halisi kiini cha Hija hiyo kufanyika mkoani Kigoma.

Akihutubia, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Alexernder Mahawe alilipongeza Kanisa Halisi kwa kuwa na maono chanya ikiwemo kuhudumia jamii na kuhimiza uzalishaji kama sehemu ya Ibada.

Mkuu huyo wa Wilaya alimuomba Baba Halisi, Kanisa hilo kuendelea kuuombea mkoa wa Kigoma ili uendelee kuwa mkoa wenye neema, Amani, Mshikamano na baraka tele na pia kumuombea Rais Samia ili aendelee kutekeleza majukumu yake makubwa kwa hekima na maarifa ili Taifa la Tanzania lisonge mbele.

Naye Sheikh wa mkonia Kigoma, Sheikh Mulamba Mussa alipopewa nafasi ya kuzungumza naye pia alilipongeza Kanisa Halisi  kwa kuijali jamii ambapo alisema katika kuijali jamii Kanisa hilo limesaidia mambo kadhaa ya maendeleo katika Elimu na Afya.

Sheikh Mulamba alimuomba Baba Halisi, Kanisa hilo kuwasaidia Waislam kupata kituo cha kulea Vijana.

Naye Katekista wa Kanisa Katoliki Kigango cha Lazaro Gasper Kaliye akizungumza baada ya kupewa nafasi,alieleza kufurahishwa kwake na namna Kanisa Halisi linavyoshughulika katika kuwajenga watu kiroho huku likihimiza Amani, Upendo na uzalishaji.

Alisema, Kigoma imebahatika kupata viongozi wenye busara na hekima kubwa kama Baba Halisi, lakini kwa bahati mbaya baadhi yao hawayashiki wanayofundishwa na viongozi hao.

"Kigoma tumebahatika kupata viongozi wenye busara na hekima, lakini tunasikia, hatusikii, sasa umefika wakati tusikie na kutekeleza tunayofundishwa na viongozi hawa", alisema Katekista huyo na kuongeza, "Kigoma tunapendwa lakini hatupendeki, lakini Baba Halisi nakuomba uendelee kutupa neno tuamke".

Mahujaji waliohudhuria Ibada hiyo wwengi wao walisafiri kwa treni ya kukodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo ilianzia safari Dar es Salaam hadi Kigoma na wengine walifika kwenye Hija hiyo kwa kutumia mabasi ya kukodi.

Akifunga Ibada hiyo, Baba Halisi alisema, Hija hiyo imeonyesha baraka kuwa kwa kuwa imeweka kuwafanya Wana wa Is-mail na Is-haka kukaa pamoja kwa kuwa kwenye Hija hivyo Wakristo na Waislam kina baba na kina mama na vijana walihudhuriwa kwa wingi na kukaa hadi mwisho wa Ibada hiyo. 

Picha:  Mtiririko wa Ibada hiyo ulivyokuwa mwanzo hadi mwisho👇

Mahujaji wakijiandaa kufanya maandamano ya amani kutokaa kwenye Kanisa Halisi la Mungu Baba la Mwanga Kigoma, kwenda kwenye Ibada maalum iliyofanyika Katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma-Ujiji.
Mahujaji wakiwasili kwa Maandamano katika Uwanja wa lake Tanganyika Mjini Kigoma-Ujiji.
Baba Halisi na Baba Halisi (kulia) wakipokea maandamano hayo.
Kuhani Moja aliyeongoza maandamano hayo akisoma Risara kwa Baba Halisi.
Baba Halisi akisikiliza wakati Risala ikisomwa.
Kuhani Moja akikabidhi risala kwa Mmoja wa wasaidizi wa Baba Halisi baada ya kuisoma
"Karibuni Mahujaji, karibuni Mahujaji", Baba Halisi akapaza sauti kuwapokea mahujaji baada ya kusomwa risala.
Baadhi ya Mahujaji wakimsikiliza Baba Halisi wakati alipopokea maandamano yao.
Waimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba 'wakilishambulia' jukwaa kwa nyimbo moto moto za kumtukuza Mungu wakati Mahujaji wakiwasili.
Waimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiendelea 'kulishambulia' jukwaa kwa nyimbo moto moto za kumtukuza Mungu wakati Mahujaji wakiwasili.
Baadhi ya Mahujaji wakiwa nje ya Uwanja wa Lake Tanganyika kusubiri Ianze saa 8 mchana.
Baba Halisi na Mama Halisi wakiwa katika nyuso za kubarikiwa wakati wakisubiri muda wa kuanza Ibada hiyo saa 8 mchana. Baba na Mama Halisi walitangulia kufika Uwanjani kwa ajili ya kupokea Maandamano ya Mahujaji. Nyuma ya Baba Halisi ni Kaka Halisi na Wasaidizi wengine.
Kuhani Moja akiwa na Kanisa (mke) wake wakati wakisubiri Ibada kuanza.
Kuhani Ushindi Halisi akizungumza jambo na Diwani wa Kigoma Mjini.
Hujaji akifurahia nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa kabla ya Ibada kuanza huku akionyesha utaifa wake kwa kupeperusha bendera za Taifa.
Kuhani Moja akizungumza na baadhi ya Polisi waliokuwa wakisimamia usalama kwenye Ibada hiyo.
Waimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiendelea kutumbuiza nyimbo moto moto za kumtukuza Mungu wakati Mahujaji wakiwasili.
Mpuliza 'domo la Bata' ambaye ni mwanamuziki nguli wa siku nyingi King Malou, akiwajibika jukwaani.
Waimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiendelea kutumbuiza nyimbo moto moto za kumtukuza Mungu.
Waimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiendelea kutumbuiza nyimbo moto moto za kumtukuza Mungu.
Muaimbaji wa Kundi la Muziki wa kutukuza Mungu Baba la Kanisa Halisi la Mungu Baba akiimba wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri.
Mahujaji wakifanya shukurani ya kugaragara mbele za Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo
Mahujaji wakifanya shukurani ya kugaragara mbele za Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Mahujaji wakiserebuka kwa shangwe wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mahujaji wakicheza kwa shangwe wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mahujaji wakiserebuka kwa shangwe wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mahujaji wakiserebuka kwa shangwe wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mahujaji wakiwa wenye nyuso za baraka kwa shangwe wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo: Mahujaji wakiwa na mtoto waliyefika naye kwenye Hija hiyo.
Mahujaji wakishangilia na bendera zao za taifa la Tanzania wakati ukipigwa wimbo wa 'Mungu Baba aliye chanzo cha mema na mazuri'.
Mahujaji wakijadiliana jambo wakati wa Ibada hiyo Uwanjani. Kulia ni Kuhani wa Morogoro.
Mahujaji kutoka Mbeya wakionyesha nyuso za tabasamu wakiwa kwenye Ibada hiyo.
mahujaji wakionyesha nyuso za tabasamu wakiwa kwenye Ibada ya Hija hiyo.
Hujaji akiwa amejipamba kwa skavu ya Beandera ya Taifa la Tanzania wakati akiwa kwenye Ibada ya Hija hiyo.
Ibada ni Uzalishaji: Kijana akitafuta wateja wa miwa, kwenye Ibada hiyo ya Hija ya Kanisa Halisi la Mungu Baba.

Mahujaji wakipunga upepo nje ya Uwanja walipokuwa wakisubiri Ibada hiyo kuanza.  

Mgeni Rasmi kuwasili👇

Kuhani Moja (kushoto) akiwa na Makuhani kutoka maeneo mbalimbali wakati wakisubiri Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma kuwasili.
Kuhani Moja akimlaki Mkuu huyo wa Wilaya baada ya kuwasili Uwanjani kwenye Ibada hiyo ya Hija.
"Karibu Sana Mheshimiwa", Kuhani Moja akasema kwa unyenyekevu. Kisha Kuhani Moja akaanza kuwatambulisha makuhani hao kwa Mkuu huyo wa Wilaya, mmoja baada ya mwingine👇
👇
👇
👇
👇
👇
👇
Mwisho wa Utambulisho👆
Kiongozi Mkuu wa kanisa Halisi la Mungu Baba akimlaki meza Kuu Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya akisalimia Mahujaji. baada ya kuwasili meza kuu. Kushoto ni Mama Halisi.
"Haya Mheshimiwa, karibu uketi", Baba Halisi akamwambia Mkuu huyo wa Wilaya.
Kisha wakaketi
Mkuu huyo wa Wilaya akimuuliza jambo kuhani moja. Kulia ni Kaimu DAS wa Wilaya ya Kigoma Maximilian Ngasa na kushoto ni Kaka Halisi.
"Sasa Mahujaji Simameni tufanye shukrani Mgeni wetu Rasmi ameshawasili", akasema baba Halisi kuwaambia Mahujaji.
Kisha Baba Halisi akaketi na kuzungumza mawili matatu na Mkuu huyo wa Wilaya.
Baba Halisi akasimama tena kwa ajili ya kufanya shukrani ya kumpokea Mgeni Rasmi.
Baba Halisi akitoa maneno ya Shukrani kumkaribisha mgeni rasmi.
Baba Halisi akiendelea na shukrani.
Watu mbalimbali wakiwemo Masheikh waliohudhuria Ibada hiyo.
Watu mbalimbali ambazo siyo waumini (Uzao) wa Kanisa Halisi la Mungu Baba waliohudhuria Ibada hiyo.
Mahujaji wakipokea Shukrani kutoka kwa Baba Halisi
Mahujaji wakipokea Shukrani kutoka kwa Baba Halisi
Baba Halisi akifanya Shukrani ya Kumwinua (kumuombea) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote. Mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na kaimu DAS wa Wilaya ya Kigoma, Baba Halisi aliwatanguliza mbele ili kuipokea Shukrani hiyo kwa niaba ya Rais Samia.
Baba Halisi akiendelea kumuombea Rais Samia.
Kisha Baba Halisi akatambulisha wageni mbalimbali.
"Unamuona yule, ni Kuhani kutoka Marekani, amepita nchi nyingi kuja kwenye Hija hii kupokea Baraka", akasema Baba Halisi.
Mkuu huyo wa Wilaya akimpungiana mkono na kuhani huyo kutoka Marekani.
Kisha baba Halisi akamwambia mtazamo wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, akasema "Sisima mtazamo wetu ni mambo matatu, Amani, Upendo usio bagua na Uzalishaji".
"Kwa hiyo katika Ibada zetu za kila siku hayo ndiyo huyasisitiza sana", akasema Baba Halisi.
Mahujaji wakimsikiliza Baba Halisi.
Mahujaji na wahudhiriaji wengine wakimsikiliza Baba Halisi, ambapo baada ya Baba Halisi kufanya utambulisho, alimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya ili awakaribishe kama mwenyeji wa Kanisa Halisi kuanza Ibada hiyo ya Hija.
Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza baada ya kukaribishwa na Baba Halisi ambaye alikuwa anamsikiliza kwa makini yote.
Kisha Baba Halisi akasimama kuonyesha kuyapokea mazuri yote aliyosema Mkuu huyo wa Wilaya.
"Asante sana kwa maneno yako uliyotupa mazuri, tumeyapokea", akasema Baba Halisi huku akimpa mkuu hiyo wa wilaya mkono wa shukrani.
Naye Mkuu huyo wa Wilaya akaipokea shukrani ya Baba Halisi kwa mikono yote.
Kisha Baba Halisi akafanya shukrani ya kupokea maneno katika Hotuba ya Mkuu huyo wa Wilaya.
"Hayo uliyotueleza ni mane makubwa nasi tutayatekeleza", akasema Baba Halisi
Baadhi ya Kina Mama na Kina Baba wa Kiislamu wakiwa kwenye Ibada hiyo,
Watu mbalimbali wakiwa kwenya Ibada hiyo ya Hija.
Afisa Usafirishaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Godfrey Siwingwa (kushoto) ni miongoni mwa viongozi wa Taasisi za Serikali waliohudhuria Ibada hiyo ya Hija. Wapili kulia ni Hujani kutoka Mtwara ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa mkoa huo.
Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ (24 KJ) naye hakupenda kupitwa japo alichelewa kidogo lakini aliweza kuhudhuria Ibada hiyo ya Hija. Hapo amelakiwa na Kuhani Ushindi Halisi.
Baba Halisi na Mama Halisi wakifurahia Wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri.
Mkuu wa Wialaya akisoma kitabu cha taarifa za Hija hiyo ya Kigoma.
Baba Halisi akifanya Shukrani katika Ibada hiyo.
MaBaba Halisi na Mama Halisi wakifurahia wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri ukiimbwa.
Vitambaa vikipeperushwa wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri ukiimbwa.
Mahujaji vikifurahia wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri ukiimbwa.
Mahujaji wakifurahia wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri ukiimbwa.
watu mbali mbali hadi wenye ulemavu wakiwa kwenye Ibada hiyo ya Hija
Mahujaji wakiwa kwenye Ibada hiyo
Mahujaji wakifurahia wakati wa Wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri.
Waimbaji wakiimba wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri.
Mahujaji wakifurahia wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri.
Baadhi ya Mahujaji wakiwa wameketi kusubiri kupokea Baraka kutoka kwa Baba Halisi
Baba Halisi akitoa Baraka kwa mahujaji na wote waliohudhuria Ibada hiyo.
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye Ibada hiyo. Kulia ni Msaidizi wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.
Mahujaji na baadhi ya Matekista wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Makuhani wakiwa kwenye Ibada hiyo
makuhani wakiwa kwenye Ibada hiyo
Sheikh Mulamba Mussa akizungumza kwenye Ibada hiyo
Katekista wa Kanisa Katoliki Kigango cha Kagongo Lazaro Kiliye akizungumza kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi, Mama Halisi na Mkuu wa Wilaya wakifurahia wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri.
Mahujaji wakifurahia wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na mazuri wakati ukiimbwa👇
👇
👇
👇
Baba Halisi na Mama Halisi mkuu wa Wilaya wakifurahia wakati ulipokuwa ukiimbwa wimbo wa Mungu baba aliye chanzo cha mema na mazuri
Hujaji akifurahi vya kutosha wakati wimbo wa Mungu Baba aliye chanzo cha Mema na Mazuri ulipokuwa ukiimbwa.
Baba Halisi akizungumza kumruhusu Mkuu wa Wilaya aondoke mwishoni mwa Ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya akiondoka baada ya Ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya akiondoka Uwanjani baada ya Ibada hiyo, huku akisindikizwa na Kuhani Moja Halisi
Mkuu wa Wilaya akipanda gari lake kuondoka Uwanja
Mkuu wa Wilaya akiagwa kwa heshima zote baada ya kupanda katika gari lake tayari kwa kuondoka.
Kuhani aliyefika Kuhuji akitokea Kenya akizungumza baada ya kukaribishwa na Baba Halisi kwa niaba ya Mahujaji wote kutoka nchi za nje.
Kisha Baba Halisi akawaaga na kuanza kuondoka Uwajani.
Baba Halisi akiondoka Uwanjani.
Baba Halisi akienda kupanda gari lake jeupe kama mavazi yake.
Baba Halisi akipanda gari lake tayari kwa kuondoka Uwanjani Baada ya Ibada hiyo.
Msafara wa Baba Halisi ukiongozwa na Polisi wakati unaondoka katika uwanja wa lake Tanganyika mkoani Kigoma, baada ya Ibada hiyo kufana.
Mahujaji wakimpungia mkono Baba Halisi wakati akiondoka na msafara wake.
Mama Mpambaji maarufu akiagalia hali ya namna alivyopamba, baada ya ibada kumalizika.

Mama Mpambaji akiwa na Mwanae katika eneo alilopamba.
Mama Mpambaji akiwa na Mwanae na Kuhani wake katika eneo alilopamba kwa uhodari mkubwa.
Kuhani Ushindi Halisi akifurahia jambo na Sheikh Mlamba ambaye alihudhuria Ibada hiyo.
©2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana