Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma wakitembelea kukagua mradi wa Hoteli ya kisasa ya Dodoma City iliyopo mkabala na Makao Makuu ya CCM Barabara ya Nyerere jijini Dodoma Machi 22, 2022.
Ujumbe huo umeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwini Mkanwa pamoja na Katibu wa CCM wa Mkoa huo, Pili Augustino.
Ujumbe huo ulipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya hoteli hiyo ambapo wengi wao walionesha kupendezewa na mradi huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Augustino akipita katika moja ya ngazi ndani ya jengo hilo ambalo pia lina ghorofa ya chini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa (katikati) akiongoza ujumbe wa kamati ya siasa kutembelea mradi huo wa hoteli inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Hoteli hiyo inatarajiwa kufunguliwa miezi michache ijayo. Kushoto ni Mchumi wa Jiji la Dodoma, Francis Kaunda.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kutembelea mradi huo wa hoteli.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment