Mwenyekiti wa Kijiji cha Makanda, Mussa Sajilo akifungua mkutano maalumu wa mafunzo ya MKURABITA kuwajengea uwezo wa matumizi bora ya Hatimiliki za Kimila kupata mikopo kutoka benki na taasisi zingine za kifedha. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha wadau mbalimbali yalifanyika katika Kijiji hicho Aprili 27, 2022.
Wananchi wa Kijiji cha Makanda, wilayani Bahi, Dodoma wametoa shukrani kwa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa jinsi ya kunufaika kupata mikopo kwa kutumia hati miliki za ardhi za kimila ambazo pia watakabidhiwa na MKURABITA baada ya kuwarasimishia mashamba yao.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Makanda, Mariam Nkondo akielezea utaratibu wa mafunzo hayo.
Wananchi wa kijiji hicho wakiwa makini kufuatilia mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bahi, Abia Silungwe akitoa mafunzo ya kilimo biashara.
Daktari wa Mifugo wa Wilaya ya Bahi, Michael Ziwa akielezea ufugaji bora wa mifugo.
Meneja Bishara wa CRDB, Gilbert Malebo akitoa mafunzo kuhusu taratibu za kupata mikopo kwa kutumia hati miliki za kimila.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi,Riuben Mtiruka akielezea kuhusu fursa mbalimbali za mikopo zitolewazo na Halmashauri.
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Bahi,Noel Samweli akitoa mafunzo kuhusu uundwaji wa ushirika na manufaa yake.
Afisa Maliasili wa wilaya, Francis Kasambala akielezea umuhimu wa ufugaji wa nyuki kibiashara
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, baadhi ya wananchi wakitoa shukrani kwa MKURABITA.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment