Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Dkt Ritta kabati ameeleza mkakati wake wa kusheherekea sikukuu ya Pasaka pamoja na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutoa sadaka katika vituo vya watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu Iringa.
Kabati ameyasema hayo wakati alipotembelea katika kituo cha watoto Yatima Cha Huruma kilichopo, Mawelewele, katika Manispaa ya Iringa katika siku ya Ijumaa Kuu.
Amesema ameamua kusheherekea sikukuu hii ya pasaka kwa kuwa pamoja na watoto hao ili kuikumbusha jamii kuwa kundi hili la watoto ni muhimu kuoneshewa Upendo kutokana na mazingira magumu wanayopitia.
Kabati amesema jamii inayosababu ya kusaidia malezi kwa Watoto hawa wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na Yatima ili kuandaa Taifa lenye Furaha na upendo siku za usoni.
Aidha Kabati kwa kushirikiana na kwaya ya KKKT usharika wa Mwenge iliyopo Dar Es Salaam kwa pamoja wameweza kutoa msaada wa vifaa pamoja chakula kwa watoto hao wenye mahitaji mengi.
Katika hatua nyingine Dkt Kabati ameahidi kutoa mualiko kwa watoto wa kituo hicho watakaofanya vizuri katika mitihani yao shuleni.
Kwa Upande wake Mchungaji mlezi wa Kituo hicho, Joyce Gandango ameseleza kuwa Jamii bado inauelewa mdogo katika utunzaji wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuamini kuwa suala hilo ni jukumu la wafadhili kutoka nchi nyingine.
Amesema malezi ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la watu wote na si la watu wa Matifa mengine kama ilivyojengeka katika mawazo ya wengi.
Mchungaji Gandango amesema watoto Yatima pamoja na wale waishio katika mazingira magumu ni watoto wenye mahitaji mengi kutokana na changamoto wanazopitia zilizopelekea wao kujikuta katika hali hiyo.
Aidha Mchungaji Joyce Gandango ameeleza kuwa huenda Taifa likapata watu wenye kulipiza kisasi ikiwemo Viongozi wa Serikali, dini na taasisi mbalimbali kama watoto wenye kuishi katika mazingira magumu hawataoneshwa upendo pamoja na kupewa ushauri nasihi.
Amesema watoto wengi waliojikuta katika hali ya kuwa katika mazingira mugumu hususani baada ya kufanyiwa vitendo vya ukatili ni watoto wenye kuhitahiji sana faraja na ushauri ili kuepuka kutengeneza Taifa lenye kulipa visasi.
Kwa Upande wao watoto wa Kituo cha Huruma Center wameshukuru msaada walioupata kutoka kwa mbunge Dkt Ritta Kabati pamoja na Kwaya ya Mwenge na kuwataka wadau zaidi kuendelea kutoa misaada katika kiyuo hicho kwa kuwa bado kina mahitaji mengi.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Kabati akizungumza wakati wakati akitoa sadaka kwa yatima....
Post a Comment