Huku baba wa Msanii huyu Mzee Zahir Ally Zorro akidai kuwa amepata tetesi kupitia mitandao ya kijamii kuwa mtoto wake Maunda Zorro amefariki Katika ajali japo hana taarifa kamili.
Nasikia watu wanamuaga Mauda Zorro mitandaoni "Lala Salama Maunda Zorro na kuweka picha take "hivyo siwezi Sema chochote ikiwa bado sijapata taarifa kamili
Huku Kaka wa marehemu Maunda Zorro ,Msanii Banana Zorro amethibitisha juu ya taarifa hizo kuwa ni kweli amefariki Dunia
Alisema Hadi jana Jioni alikuwa na Maunda kwenye msiba wa rafiki yao ila Jioni alipata taarifa kuwa Maunda amefariki Kwa ajali .
"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospital Kigamboni ,taarifa ni za kweli tulikuwa kwenye msiba wa rafiki yetu mwingine wa karibu na Maunda hadi Jioni kati ya Saa 11 ama 12 hivi nimerudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangamo Kwa taarifa zaidi Kuhusu msiba ni hadi nimefike Hospital "alisema ajali ilitokea Saa 4 usiku
Post a Comment