Featured

    Featured Posts

CCM YAPIGA MARUFUKU VIONGOZI WAGOMBEA KUSIMAMIA UCHAGUZI+video

 



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amepiga marufuku wagombea nafasi za uongozi ndani ya chama nchi nzima ambao ni viongozi kutohusika katika mchakato wa kutoa fomu au kusimamia uchaguzi na badala yake chama kiteue mtu mwingine wa kuusimamia ili kuweka mazingira ya haki na usawa kwenye uchaguzi.


Kauli hiyo ameitoa leo mkoani Shinyanga wakati akianza ziara yake katika mkoa huo yenye malengo matatu yakiwemo Kuhimiza Uhai wa Chama ngazi ya mashina na kuzungumza na wanachama na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahudiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.


Katibu Mkuu ameeleza kuwa, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama,  hivyo wagombea ambao kwa sasa ni viongozi ngazi zote hawapaswi kusimamia uchaguzi ili hali wao ni sehemu ya wagombea na kutaka wakae pembeni kuanzia mchakato wa awali wa ugawaji wa fomu, mpaka vikao vya kupitisha wagombea ili kuwepo na uchaguzi wa haki, usawa  na huru kwa wagombea wote.


"Mwaka huu ni wa uchaguzi, fomu zitolewe kwa wogombea wote na pale ambapo kiongozi yoyote ndani ya chama anawania nafasi ni marufuku kuhusika kwenye mchakato wa uchaguzi, wabaki kuwa wagombea kama wanachama wengine ili haki itendeke, na hii ni kwa nchi nzima," amesema Ndg. Chongolo.


Katibu Mkuu amefafanua kuwa, kama Katibu wa ngazi husika anagombea kamati ya siasa ichague mjumbe mmoja miongoni mwa wajumbe asimamie uchaguzi, na kama Kamati nzima ya siasa inagombea, ngazi ya juu iteue kiongozi mmoja asimamie uchaguzi huo ili kujiepusha na ujanja ujanja wa baadhi ya viongozi wagombea kuficha fomu kwa baadhi ya wagombea wenzao  kwa maslahi yao binafsi badala ya chama.





 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana