Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akitoa maelekezo Kwa Dk Nicodemus Senguo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga wakati alipokagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali ya wilaya hiyo inayojengwa katika Kijiji Cha Mtonga kata ya Nyamilangano kulia ni Kanali Lubinga Ngemela Katibu wa NEC Saiasa na Ushirikiano wa Kimataifa CCM.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -USHETU)
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufanikisha upelekaji wa vifaatiba katika Hospitali ya Wilaya ya Ushetu ili ianze kutoa huduma.
Chongolo ameyasema hayo leo, Mei 28, 2022 wakati akikagua jengo la Hospitali ya Wilaya ya Ushetu wakati wa ziara yake katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu
Katika maelekezo yake Chongolo amesema pamoja na Sh48 milioni zilizolipwa kwa MSD kupeleka vifaa hivyo, pia kuna mgao wa vifaatiba kutoka Serikali kuu akihoji nini kinachelewesha kupeleka vifaatiba hivyo.
“Nimesema nitakachofanya nitazungumza na Waziri wa Afya (Ummy Mwalimu), lakini nimemuelekeza Mkuu wa Mkoa (Sophia Mjema) kumtafuta muhusika wa MSD eneo hili ili kesho (leo) nikutane naye.
Amesema mazungumzo yake na mamlaka hiyo yanalenga kupata jawabu la hatua za haraka zitakazochukuliwa na bohari hiyo kuhakikisha vifaatiba vinapatikana katika Hospitali hiyo.
Ujenzi wa hospitali hiyo umetetekelezwa Kwa awamu tatu na ulianza Januari 2019 ambapo serikali imepeleka fedha jumla ya shilingi bilioni 3.1 Kwa ajili ya kukamilisha.
Post a Comment