Featured

    Featured Posts

MITAHANI YA KIDATO CHA SITA NCHINI KUANZA LEO, MEI 9 HADI MEI 27 MWAKA HUU

 Na CCM Blog, Dar es Salaam
Jumla ya Watahiniwa 95,955 kutoka shule 841 za sekondari na vituo vya kujitegemea 250 wanatarajia kufanya mitihani yao ya kumaliza Kidato ya Sita, kuanzia leo Jumatatu Mei 9, 2022 hadi Mei 27, 2022.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika Ofisi za Baraza hilo la Mitihani, Jijini Dar es Salaam.

Dk. Msonde amefafanua kuwa, watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya Stashahada na cheti.

Amesema, kati ya watahiniwa wa Kidato cha Sita 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

"Kati ya hao wanaume ni 47,859 sawa na asilimia 55.96 na wasichana ni 37,672 sawa na asilimia 44.04, watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 151 na kati yao 136 ni wenye uoni hafifu na 15 ni wasioona,"amefafanua.

Amesema, kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,424 waliojisajili, wanaume ni 6,546 sawa na asilimia 62.80 na wanawake ni 3,878 sawa ana silimia 37.20 na asiyeona ni mmoja.

Pia amesema, kati ya walimu wataketi kufanya mtihani huo, 4,560 ni ngazi ta stashahada na 5,110 ni ngazi cheti.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana