Featured

    Featured Posts

MUSOMA VIJIJINI KUANZA KUWA NA HIGH SCHOOLS ZA SAYANSI

 



Jimbo la Musoma Vijijini linayo HIGH SCHOOL moja tu, nayo ni ya masomo ya ARTS (HKL, HGK na HGL). Hii ni Kasoma High School iliyoanza Mwaka 2014, na ni sehemu ya Sekondari ya Kasoma iliyofunguliwa Mwaka 1995. 


Jimbo letu lina jumla ya:


*Sekondari 22 za Kata/Serikali

*Sekondari 2 za Binafsi (Madhehebu: Sabato & Katoliki)


Wananchi ndani ya Kata 21 za Jimbo letu wamepanga na wengine wameanza ujenzi wa Sekondari Mpya 10 - moja (Ifulifu Sekondari) ikiwa imepokea kutoka Serikalini Tsh MILIONI 470 za ujenzi wa Sekondari ya Kata hiyo itakayofunguliwa Juni 2022.


UJENZI  NA UBORESHAJI WA MAABARA


WANAVIJIJI, kwa kushirikiana na SERIKALI yetu, wameamua kujenga na kuboresha MAABARA zote za Sekondari zetu. MAABARA hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.


Mbali ya kuboresha uelewa na ufundishaji wa masomo hayo kwa WANAFUNZI wa KIDATO cha I hadi IV, lengo jingine ni kuanzisha HIGH SCHOOLS za MASOMO ya SAYANSI (k.m., PCM & PCB) Jimboni mwetu.


Tumepanga tuwe na High Schools angalau 5 za masomo ya sayansi ifikapo 2025.


WANAVIJIJi wa Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 wameamua kujenga MIUNDOMBINU ya HIGH SCHOOL ya masomo ya SAYANSI - tafadhali wasikilize kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.


SHUKRANI zinatolewa kwa:

*Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan

*Benki za NBC, NMB, CRDB na TPB

*Baadhi ya Wazaliwa wa Kata ya Kiriba


Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu:

https://ift.tt/Ounf6Fi


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

https://ift.tt/Ounf6Fi



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana