Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima Bw. Hassan Milanga mara baada ya kupokelewa katika kata ya Nkoma Itilima Leo , Chongolo anaendelea na Ziara yake Mkoa wa ambapo amewasisitizia Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia changomoto ya Tembo kuharibu mazao ya wakulima pamoja na makazi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Combred Daniel Chongolo akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Itilima akiwa katika Ziara yake Mkoa wa Simiyu kwa kupokelewa Wilayani Itilima kata ya Nkoma
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Combred Daniel Chongolo akisalimiana na viongozi mbalimblai akiwa kwenye Ziara yake Mkoa wa Simiyu kwa kupokelewa Wilayani Itilima kata ya Nkoma.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu akimuaga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya kumaliza ziara yake wilayani Meatu na kuanza wilaya ya Itilima Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohammed na wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Itilima Faidha Salim.
…………………………………
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amemtaka mbunge wa Jimbo la Itilima Njelu Silanga kuwawezesha wakulima wa Jimbo Hilo kuhakikisha Kila tarafa wanapata Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti Ili kuongeza thamani ya zao hilo ambapo kwa Mkoa wa Simiyu, Itilima inaongoza kwa uzalishaji wa alizeti.
“Najua Mbunge wenu ana wajibu wa kuwasaidia mashine za kuchuja mafuta ya alizeti, wasaidie wananchi Hawa wapate mashine za kuchuja mafuta ya alizeti angalau kwa mashine moja kwa Kila tarafa na hili litawasaidia sana kuongeza thamani ya zao hili.”
Katibu Mkuu ameongeza kuwa kitendo Cha kufunga mashine, wakulima wataanza kuuza mafuta badala ya kuuza alizeti zenyewe, ambapo kwa sasa mafuta ya alizeti ndio mafuta bora na ghali zaidi, hivyo wananchi watapata fedha za kutosha tofauti na sasa.
Post a Comment