Mwakata, Shinyanga
Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata Barabara ya Isaka-Kahama mkoani Shinyanga.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea muda wa saa 4 usiku Jumatatu Agosti 8, 2022, ikihusisha gari aina ya IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta.
Imeelezwa kuwa Hiace iligongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamefadiki na wengine 15 kujeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo.
"Watu 17 walifadiki papo hapo eneo la tukio na wengine watatu walifariki baada ya kufikishwa hospitali, majeruhi wapo 15", taarifa imeeleza.
Hadi tunaandika habari hii Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga lilikiwa halijazungumza kuhusu ajali hiyo. juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi zinaendelea. (Sorce: Mitandao)
Post a Comment