Featured

    Featured Posts

BALOZI WINFRIDA SHONDE ATOA RAI KWA WATANZANIA KUJITOKEZA KUHESABIWA SIKU YA SENSA KESHO AGOSTI 23, 2022

Kigamboni, Dar es Salaam
Mshauri Elekezi na Balozi wa Mazingira Winfrida Jackson Shonde ametoa rai kwa Watanzania kujitokeza katika kuhesabiwa kesho August 23, 2022 kwakua Hesabu hiyo ndiyo itakayopelekea kuirahisishia Serikali katika mambo mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kupanga bajeti katika Wizara mbalimbali na kusaidia maendeleo kwa taifa na watu wake.

Pia ameeleza umuhimu wa Sensa upande wa Mazingira utasaidia mikakati thabiti ya kufanya tathmini ya athari za mazingira na kuweka mikakati thabiti kuzuia au kupunguza athari za mazingira zitikanazo na shughuli za binadamu ambapo kujulikana kwa idadi ya watu kutalifanya Taifa kujipanga vyema na kuweka Miundombinu /mikakati inayoendana na Uhalisia.

Ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Juhudi za kuhamasisha zoezi hili na kuendelea kusapoti juhudi zinazofanywa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Ameyasema hayo Katika Hamasa ya Sensa Wilaya ya Kigamboni Iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya Kigamboni Fatma Nyangasa na kuhudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wadau pamoja na wananchi wa Kigamboni. Tafadhali msikilize, HAPO👇
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana