Alhamisi, 18.8.2022, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alikuwa Kisiwani Rukuba kwenye Kampeni ya Sensa ya Watu na Makazi
Mbunge huyo aliambatana na Diwani wa Kata ya Etaro, Mhe Emmanuel Kigwa. Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Etaro.
Kabla ya kufanya Mkutano wa Uhamasishaji wa ushiriki kwenye SENSA ya tarehe 23.8.2022, Mbunge huyo alikagua ujenzi wa KITUO cha AFYA cha Kisiwa hicho.
Serikali imeishatoa jumla ya Tsh Milioni 500 (Tsh 500m) kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha Afya.
Ujenzi unaendelea vizuri na majengo yaliyokamilishwa kwa zaidi ya asilimia 80 (80%) ni:
*Maabara
*Wodi ya Mama na Mtoto
Wana-Rukuba wamedhamiria kukamilisha ujenzi wa Kituo chao cha Afya ifikapo mwishoni mwa Oktoba 2022.
Shukrani nyingi sana zinatolewa kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan. Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
Wakazi wote wa Kisiwa cha Rukuba wako tayari kuhesabiwa, na wameahidi kushiriki kwenye zoezi la SENSA ya Watu na Makazi kwa asilimia moja (100%).
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
https://ift.tt/vgazr6b
Post a Comment