Featured

    Featured Posts

MILIPUKO YASIKIKA MJINI KHRKHIV USIKU KUCHA

Msururu wa milipuko ilisikika katika mji wa Kharkov Jumapili jioni na kulingana na vyombo vya habari vya ndani, kulikuwa na takriban milipuko 10 kwa jumla iliosikika.

"Ni sauti kubwa sana zinazosikika. Ninaomba kila mtu aende kwenye makaazi. Ukiwa nyumbani, fuata ushauri wa kuta mbili," Meya wa Kharkiv Igor Terekhov aliandika kwenye mtandao wake wa telegram.

Muda mfupi kabla ya sauti hizo za milipuko kusikika tahadhari ya uvamizi wa anga ulitangazwa jijini, na nchini kote.

Taarifa zinasema,  Meli nne za mizigo zilizo na nafaka na bidhaa zingine za kilimo ziliondoka kwenye bandari za Ukraine. Baadaye, meli nyingine iliingia kwenye bandari ya Ukraine ya Chornomorsk ili pia kubeba bidhaa za kilimo.

Mashambulio dhidi ya mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhya yameendelea na kuna hatari ya kuvuja kwa mionzi. Wahusika kwenye mzozo wanalaumiana.
     
Katika eneo la Nikolaev takriban kuna watu waliouawa na wengine watano kujeruhiwa kufuatia mashambulizi.
Uswidi itajiunga na nchi kadhaa za Magharibi kuwafunza wanajeshi wa Ukraine na imesema itatuma wakufunzi 120 kwenye kambi za kijeshi nchini Uingereza kushiriki katika mpango huo unaoongozwa na Uingereza.
  Athari za milipuko hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana