Ikulu, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala kuwarudisha mafunzoni Maafisa na Askari waliopo kazini kupata mafunzo tena chuoni hapo.
Pia amelitaka Jeshi la Uhamiaji kuondoa urasimu wa utoaji vibali vya kuingia nchini (Visa) kwa wageni, akisema Idara hiyo haina sababu ya kuchelewesha wageni kupata vibali vya kuingia nchini kwa kuwa wanatumia mifumo ya kisasa ya kielektroniki katika utoaji wa vibali hivyo.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Jeshi la Uhamiaji Kozi na. 1/2022, katika Chuo cha Uhamiaji cha Boma Kichakamiba.
Pia, Rais Samia ametaka kuwepo kwa mafunzo baina ya vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini ili kupata uzoefu wa pamoja.
Rais Samia amelitaka Jeshi la Uhamiaji kubuni njia mbalimbali zitakazosaidia kuimarisha utendaji ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia na mbinu mpya za uhalifu zinazojitokeza.
Haya ni mafunzo ya kwanza kwa Uhamiaji tangu kuanza kujitegemea kwa Jeshi hilo ambapo Askari wa uhamiaji 818 wamehitimu na mafunzo hayo kupewa jina la Operesheni Ujenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kabla ya kufungua Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji katika Hafla iliyofanyika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Post a Comment