Ikulu, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameateua Mkuu wa mkoa wa Singida Mstaafu Binilith Satano Mahenge kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Longinus Rutasitara ambaye alimaliza muda wake.
Taaraifa ilyotolewa na Ikulu, imesema pia Rais amemteua Prof. Aurelia Kokuletage Ngirwa Kamuzora, Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Festus B. Limbu ambaye alimaliza muda wake.
Taafa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus imsema uUteuzi huu ni kuanzia tarehe 11 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan |
Post a Comment