Featured

    Featured Posts

RUTO ASHINDA URAIS KENYA

Nairobi, Kenya

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha UDA nchini Kenya William Ruto ndiye Rais mteule nchini humo.


Ruto ameibuka mshindi baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Raila Amollo Odinga wa Muungano wa Azimio baada ya kupata kura 7,176,141 dhidi ya mpinzani wake mkuu aliyepata 6,942930.


Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Bomas , mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati amesema kwamba Ruto amejipatia asilimia 50.49 ya kura naye Raila akaijipatia asilimia 48.85.


Vilevile mgombea wa chama cha Roots Party George Wajackoyah alipata 69969 huku mwenxzake wa chama cha Agano Waihiga Mwaure akijipatia 31987.


Ruto ametangazwa mshindi huku kukiwa na mgawanyiko baada ya mgombea wa Muungano wa Azimio kususia sherehe ya kumtangaza mshindi.


Makamishna wanne wa tume hiyo walizungumza na waandishi wa habari wakidai kwamba hawataki kuhusishwa na matokeo hayo kutokana na jinsi shughuli ya uchaguzi ilivyoendeshwa.


Akizungumnza katika hotuba yake punde baada ya kutangzwa mshindi , Bwan Ruto alisema kwamba angependa kumshukuru Mungu kwa kunifikisha katika hatua hii.


''Najua kwamba baadhi ya watu walibashiri kwamba hatutafika hapa lakini kwasababu kuna Mungu Mbinguni tumefika. Shukran zangu ziwaendee Wakenya wote''.


Awali akimtangaza mshindi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati alisema: Tumetembea safari ya kuhakikisha kwamba Wakenya wanashiriki katika uchaguzi ulio huru na wa haki.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana