New York Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo na namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa na namna ya kuendeleza sekta za uchukuzi, muindombinu, kilimo, biashara na uwekezaji nchini.
Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya kuongeza ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa na kuihusisha sekta binafsi katika harakati za kuinua uchumi wa Tanzania.
Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi hizo.
Viongozi hao wajadili namna wanavyoweza kushirikiana kupitia sekta ya biashara, uwekezaji na uchukuzi na hivyo kuchangia harakati za ukuzaji wa uchumi wan chi hizo.
Viongozi hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia kitabu cha taarifa alichopatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri Mulamula alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao.
Post a Comment