Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa Bunge Sports, Tarimba Abbas zitakazotumika wakati wa Bonanza la Kivumbi na Jasho litakalofanyika kesho Jumamosi Septemba 17, 2022 kwenye viwanja vya Chinangali Park na Kilimani jijini Dodoma.
Bonanza hilo linalodhaminiwa na benki hiyo litazishindanisha timu za bunge na benki ya NMB.Zaipuna na Tarimba wakiwa pamoja na baadhi ya wabunge wakionesha jezi za Bonanza hilo.
Zaipuna, Tarimba na Ester Matiko wakiangalia fulana itakayovaliwa wakati wa matembezi kutoka eneo la Bunge hadi viwanja vya Chinangali Park.
Tarimba akizungumza na vyombo vya habari kuelezea Bonanza hilo huku akisikilizwa na Zaipuna
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Zaipuna akikabidhi vifaa na jezi kwa ajili ya bonanza hilo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment