Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dodoma
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kimefanya Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya kawaida vya Uongozi ngazi ya Taifa ambavyo pamoja na mambo mengine vina kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama ambao wameomba uongozi wa Chama katika ngazi ya wilaya.
Kikao hicho cha leo cha NEC kilimetanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CC) kilichofanyika jana, Ikulu chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan na Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika tarehe 22 na 23 Septemba, 2022 Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Kikao hicho Maalum cha NEC ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Saamia, kimehudhuriwa na viongozi wote wa Kitaifa wa CCM wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Mjumbe wa Kamati Kuu Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye Kikao hicho. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akihamasisha Wajumbe wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kuingia ukumbini kwenye kikao hicho. Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan akifurahi baada ya kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassani na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakipiga kofi la shangwe baada ya kuingia ukumbini. Viongozi wakiwa wamesimama kumlaki Mwenyekiti Samia
Viongozi wakiwa wamesimama kumlaki Mwenyekiti Samia
Hali ya ukumbini
Wajumbe wakiwa wamesimama kumlaki Mwenyekiti Samia
Post a Comment